Kuna watu bwana vyakula vingine hawawezi kula au kuchanganya anahisi atatapika

Mkogoti

TAPELI Mkubwa
Joined
May 3, 2020
Posts
2,415
Reaction score
3,924
Kama Mimi kuna jamaa zangu mmoja hawezi kula ndizi mbivu anahisi atatapika, mwingine huyo anasema akila wali na soda basi lazima arudishe basi fuluuu raha unakuta mimi nafurahi kweli nasombelea tu,

Ila mimi sasa nikila samaki na chai hapo naweza kutapika vyote maana nahisi kichefuchefu na mimi ni Mwanaume 😜😁 maana najua kuna watu humu watakuja na yao,

Ebu tuelezane wewe naona ukichanganya chakula gani na gani basi havitaki kukaa tumboni.


🀦πŸ€ͺπŸƒ
 
Hapo kwenye kichefuchefu hebu uendee hospital ukapime yawezekana yaliyomo yamo
 
Nyama yoyote ichanganywe na njegere..natapika

Kuna video ya AT (nipigie)..nikiangalia ile video ikifika sehemu yule dada anapakua mboga imechanganywa njegere na kuku siangalii..maana naona kutapika kunakuja.
 
Mchanganyo wa dagaa mwanza au kigoma kwa chakula chchte, yaani nikiona tyuuuh hat km sijala natapika.
 
Tafuna dagaa wakavu kisha kula karanga mbichi (i.e. kavu lakini hazijakaangwa) uone habari yake. Hii ni universal, haichagui. Kila mtu lazima chenji irudi.
 
Mchanganyo wa dagaa mwanza au kigoma kwa chakula chchte, yaani nikiona tyuuuh hat km sijala natapika.
We mshamba. Kaanga dagaa wa Kigoma kwenye mafuta kisha changanya na maharagee yaliyokwisha iva. Amin amin nakwambia, hutatamani mboga ingine Wallah tena!
 
Mkuu wewe kama mimi,mimi kutapika ni kazi sana ile kuna kichefuchefu huwa napata nikila wali dagaa wa mwanza kwa wali hakielezeki
ile harufu inachefua mkuu. Japo wengine wanakula bila shida ila kwangu siwezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…