Pole sana ndugu, lakini hilo ni tatizo dogo sana, na unalikuza zaidi katika akili yako linazidi kukuvuruga kumbe ni katatizo kadogo sana.
Nikushauri uanze tiba ya asili ya kubadilisha kabisa mfumo wako wa chakula pamoja na usafi wa meno.
1. Upe mwili wako nafasi ya kujitibu kwa kuachana na vyakula vinavyozalisha sulphur au vinavyosababisha harufu kuzidi maradufu kama vile nyama nyekundu, mayai, vitunguu nk. Na badala yake ule matunda na mbogamboga tupu angalau kwa miezi mitatu. (Na pia kama ulikuwa unameza madawa yoyote achana nayo).
2. Usinywe kabisa soda na vinywaji vyovyote vya kiwandani au vilevi na badala yake kunywa maji mengi sana angalau lita nne kwa siku na hata zaidi ya hapo.
3. Usitumie dawa za meno zenye flouride, na ikiwezekana tumia baking soda kwa kusukutulia angalau mara tatu kwa siku au zaidi ya hapo kwa kila baada ya mlo.
4. Sugua ulimi mpaka kwenye koromeo kule ndani kabisa na kwenye kuta zote za tonsils, na pia sugua juu kwenye PAA la mdomo, pembezoni na mdomo na kuzunguka fizi zote.
5. Chukua uzi wa kushonea nguo ingiza katikati ya meno safisha meno yote mpaka kwenye magego, ingiza katikati kila mahali.
6. Koroga maji ya chumvi fanya kama unayabwia mdomoni na kuyasukutua kisha yateme na meza kidogo kila siku baada ya kusukutua.
7. MAJI, MATUNDA, MBOGA ZA MAJANII ongeza kwa wingi sana.
8. Sali na fanya maombi. Nguvu za giza zipo.
9. Kila siku asubuhi unapoamka chukua malimau mawili makubwa yabinye kwenye kikombe cha maji kunywa. Kila siku angalau kwa miezi miwili uone hali ikoje.
10. Mwisho, fanya zoezi la kisaikolojia kwa kupuuza maneno na fikra za watu. Jiamini na endelea kujitibu. Hakuna aliye mkamilifu.