Kuna watu huwa wana enjoy zaidi ile hali ya wao kujulikana wameishiwa hela

Kuna watu huwa wana enjoy zaidi ile hali ya wao kujulikana wameishiwa hela

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Kuna Wale Watu wa kujichanganya na watu wa namna zote wenye hela na wasio nazo, wanywa bia na wanywa gongo huwa wananifurahisha sana pale wanapopata hela yaani moyo hautulii mpaka hela iishe.

Na kati ya maskini na matajiri nimejifunza wanaoongoza Kwa dharau ni maskini hawahawa wanywa gongo yaani mtu wao akiishiwa hela wanaanza kumcheka live live achilia mbali kumsengenya wanamchana bila kupepesa kwamba akiwa nazo huwa anawakimbia anakwenda kwenye viti virefu kula bia na kitimoto zikiisha ndo anarudi kwao hata kama huwa anawanunulia sana.

Ila sasa utashangaa mtu anapondwa hivyo lakini ndo anazidi kupenda maneno hayo ya vijembe huku akiwaomba omba yaani maisha yale ya kuunga unga kipindi anasubiri michoro mingine ye ndo anenjoy zaidi kumkopa kopa muuza pombe kudharaulika
 
Back
Top Bottom