Mimi Saa 4 hadi Saa 7 nitakuwa Karimjee Hall Kumuaga Uncle wangu Mzee Wakili Nimrod Elirehema Mkono pale Karimjee Hall kama Ratiba yake inavypsema.
Hata huyo Mzee Juma sidhani kama Keshokutwa atakuwepo pale Kijiweni Kwake ( katika Baa yake ) na Ndugu zangu Wengine Wote kwani Msiba huu wa Mzee Mkono unatuhusu Wazanaki Wote kuanzia wa Butuguri, Busegwe ( Kwao Marehemu ) na Butiama ( kwa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere )
Mwili wa Mzee Mkono unaingia Kesho Saa 11 za Alfajiri pale JNIA na utapelekwa Kwake Nyumbani Masaki kisha kutakuwa na Ibada ya Kuuombea na Sabato huku Waombolezaji wakila.
Jumapili Saa 3 Mwili utapelekwa Karimjee Hall kwa Shughuli za Kuagwa na Watu Kumzungumzia Mema yake Marehemu alipokuwa Hai.
Saa 8 Mchana Mwili utapelekwa JNIA na Saa 11 Jioni utasafirishwa kwenda Mwanza na Saa 1 Usiku utapokelewa na kuanza Safari ya kwenda Busegwe Mkoani Mara ( Uzanakini ) Nyumbani kwa Marehemu ambapo Utalala hapo.
Jumatatu Alasiri Shughuli za Kumpumzisha Wakili Msomi na Uncle wangu Mzee Nimrod Elirehema Mkono katika Nyumba yake ya Milele zitaanza na atazikwa rasmi mida ya Saa 10 za Jioni.
Rest in Eternal Peace Uncle N Mkono.