Kuna watu wagumu kuelewa

Kuna watu wagumu kuelewa

Unakuta mtu sio Mme/mpenzi/wazazi au sio mtu wa karibu sana na wewe akipiga simu anapiga weee ,hivi huwezi jiongeza ukapiga simu Mara moja mtu hajapokea ukaacha na ukasubiri akutafute mwenyewe,basi itapigwa simu kama ndio hujisikii kupokea unapunguza sauti maana ni kelele,mpigie mtu Mara moja hajapokea acha tuma sms ,haunidai,hatuna biashara nawe kwanini upige sana simu na saa ingine ukipokea ni salam tu na kuulizana maswali ,inakera kweli kweli.
Alie na haki ya kupiga simu hata Mara mia ni Mme/mke/ mpenzi/wazazi ni watu wa muhimu sana labda na baadhi ya ndugu zako maana sio ndugu wote mtaongea sana kwa simu .

Mpenzi wangu ana haki ya kunitafuta muda wowote saa yoyote,atume sms muda wowote ana haki si mnajua tena laazizi mkali ini [emoji12] [emoji12] [emoji12] ,wazazi wangu lazima nipokee,kuna rafiki zangu kama watatu lazima nipokee wengine msipopokelewa msipigepige simu

Wengine wanapenda sana kuchart kwa sms basi atatuma sms siku kucha si mchart na wapenzi wenu bana
mi uzuri huwaambia nachoka kuchart bora nipige tuongee yaishe,mwingine nishamuambia hapa siwezi kila saa najibu sms ,sms zenyewe sio za Mpesa basi kero tupu

Wengine sasa hapa wanaudhi kama nini wanapiga WhatsApp call yaan jamani si andika tu sms tu tutaona tutajibu ,ukipokea ni salaam tu hakuna la maana zaidi anataka akusalimie si uandike tu ,watu tubadilike jamani hizo salaam andikeni najua sio Mimi tu naekereka wengi tu wanakereka na hii Tabia wanashindwa kusema,sio kila WhatsApp call utapokea

kuna wa hawa wa video call hawa sasa huwa nawakatia kabisa ,na wala sijibu
ni kero ndogo ndogo tu lakin zinakera ,mim kuna siku tu sipendi kuongea na simu za watu wengine zaidi ya laazizi,rafiki zangu wawili na mama yangu wengine sipokei maana sio lazima kupokea hatuna ishu za maana za kuongea

Basi huwaga nikikuta WhatsApp call halaf sio ya mtu ambae nampenda nasonyaaa na sipokei naendelea na safari zangu,nikikuta simu inapigwa halaf sio ambayo nataka nasonyaa msonyoo mrefu naendelea na mambo yangu,nikikuta sms ya salaam ntajitahidi kujibu lakin ukiendelea kunichatisha nakaa kimyaa

ndio hivyo nishasema hutaki pasuka

Pasaka Njema wanajf
Dinazarde[emoji8] [emoji8] [emoji8]
Kama nakudai na tarehe ya ahadi imefika utanisamehe tu
 
Yan mm kuna huyo kikaragosi ananifukuzia huu mwaka wa 4 ni msumbufu hakat tamaa kazi yake kupiga sm kutuma sms sjibu hat miez lakin hachoki

Namblock lakin anabadilisha namba sjui watu wengine huwa mapopoma wanakera sana mtu hana ushirikiano anasumbua tu.
Kweli uzuri wa kitu upo machoni mwa mtu..! Pole yake anayeanfaika 4yrs sababu ya penzi la kiporo..
 
Back
Top Bottom