Kuna watu wakarimu dunia hii

Kuna watu wakarimu dunia hii

Wiki iliyopita nilisafiri kwenda Tanga, nilipanda basi la Raha Leo. Pembeni yangu alikaa mwanaume amenizidi miaka kama 10 hivi. Nilikuja kugundua baadae ni m-Pakistan na Kiswahil aliongea kidogo sana.
Jirani yangu huyu alikaa siti ya dirishani. Alikuwa amejiandaa kweli kwa safari. Alikuwa na mfuko wa makula kula. Kwenye mfuko alikuwa na meat chops, biscuits, chocolate, juice.

Tulipifika Chalinze nilimuomba aninunulie korosho kwani yeye alikuwa amekaa dirishani, ndipo nilipogundua uwezo wake wa lugha ya Kiswahili.

Alipoanza kutoa vyakula, alinikaribisha meat chops, nilijibu asante, kabla ya kutoka nyumbani nilipiga breakfast ya nguvu na nilijua lunch ya ugali na mchunga inanisubiri kwangu mimi korosho zilitosha.

Baba huyu roho yake ilisononeka sana kwa kukataa kwangu kula chakula. Alinipa chocolate, ilibidi niichukue kumridhisha.

Aliniacha hoi, alipofungua box la juice na kuniambia nianze kunywa mimi kwani anajua akianza yeye mimi sitakunywa. Nilimuomba kuwa mimi ni mzima, nilikuwa na chupa ya maji nikamionyesha huku nikimfahamisha kuwa ninapunguza matumizi ya sukari, kwangu mimi maji ndiyo mpango mzima.

Huu ni Mfano wa gentleman ambao wamebaki wachache sana.
Vipi mkuu, alikupatia hela ya tax muda wa kushuka?

Halafu, hivi kwanini wanawake mnawaza kufanyiwa u gentleman tu, kwani nyie ni dhambi kufanya u gentlewoman kwa wanaume?
 
Ndio maana huwa mnaliwa hovyo hovyo nyie!
 
Vipi mkuu, alikupatia hela ya tax muda wa kushuka?

Halafu, hivi kwanini wanawake mnawaza kufanyiwa u gentleman tu, kwani nyie ni dhambi kufanya u gentlewoman kwa wanaume?
Ahahaha watoto Wa kike wanapenda kujaliwa au kukarimiwa
Kuna sehemu nipo nawafungulia sana milango wabebez Wa kituruki na kiarabu!! Tukikutana milangoni
 
Kuna mwenzako yeye alikaribishwa chocolate, zile snickers wakati anasafiri toka Arusha kwenda Dar.. Alizundika akiwa MNH na sumu kali mwilini. Sio karne ya kukubali vitu toka kwa stranger.
 
Back
Top Bottom