Morgan Freeman
Member
- Mar 14, 2015
- 85
- 105
Wasalaam wadau,
Wakati fulani katika awamu ya tano, kiliibuka kikundi cha kusifu na kuabudu viongozi hata kufikia kutaka kubadili katiba ili kuwaongoza muda viongozi walio madarakani, sio nia ya bandiko langu kutweza utu au legacy ya hayati mwenyekiti wangu Dkt. JPM bali kuwakumbusha waabudu wale kuwa vichwa vina matumizi yake zaidi ya kufugia nywele na kwamba hakuna tumbo la kiumbe yoyote lenye ubongo uamuapo kuliendekeza litakupoteza.
Swali la msingi sana waliloshindwa kujibu mumiani wale ni je, tulikua tunarekebisha katiba zetu za chama na nchi kwa ajili ya Dkt John Pombe Magufuli au Rais Dkt. John Pombe Magufuli?
Kimsingi mumiani wale hawakujua nia ya dhati ya kile wakitakacho na matokeo yake leo hii wamebaki kubweka baada ya kuona dalili za kufa kwa matarajio yao yote, mfano mmojawapo unaoatoa kamasi ndugu zangu hawa ni utaratibu wa upatikanaji wa wagombea wa nafasi za ubunge na ndani ya chama ambapo baada ya kubadilika kwa kanuni za uchaguzi za chama, sasa kikao chenye mamlaka ya mwisho kuamua nani agombee ni kile kinachoongozwa na mwenyekiti taifa tena hata awe na kura sifuri kwa vile tu atakua na sifa njema machoni pa mwenyekiti basi atatoboa kama walivyopita ndugu zetu wabunge baadhi wanaodemka bungeni mule.
Jambo la pili linalowatia kichaa ndugu waabudu ni uchaguzi wa ndani ya chama mwakani ambao kwakweli kutokana na msiba mzito wa mwenyekiti aliyepita uliokuja ghafla kabla hata upangaji wa safu mpya 2022 na mabadiliko ya taratibu za uchaguzi ndani ya chama zinazompa leo hii mwenyekiti mamlaka makubwa ya kuamua nani awe wapi praise wengi wamevurugwa kwelikweli.
Kiujumla kutokana na ujuaji mwingi na kutokufikiri kwa upana majority ya waabudu walichonga majeneza yao wenyewe na kufunga maturubai ya misiba yao kwa kutokufikiri kuwa katiba haimuhusu mtu mmoja bali jamii nzima ni jambo la kumshukuru MUNGU kuwa katiba ya nchi haikubadilishwa laiti kama ingekua imebadilika na yakatokea ya kutokea sijui leo hii wangekua na hali gani.
NB: TUKUMBUKE KABLA YA MTU KULIKUA NA MTU NA BAADA YA MTU KUNA MTU