RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
Mhadhara - 42:
Kuna watu katika jamii wana tabia zinazofanana na hawa wanyama/wadudu.
1. PIMBI (Harakati zisizo na maana) - Wapo watu ambao wanaweza kufananishwa na pimbi. Ukikutana nae barabarani yupo race utafikiri anakwenda kuokota burungutu la hela, lakini hana anachokiwahi, busy for nothing.
2. NYEGERE (Wivu uliopitiliza) - Wapo watu ambao wana wivu kupita kiasi. Mkewe akirudi sokoni ananusa nguo za ndani za mkewe....Mwingine akifua nguo za mumewe lazima azinuse pale mbele.
3. KOBOKO (Hasira nyingi wakati wote) - Tuna watu ambao wapo kama Koboko, muda wote ni wakali, vibuli, jeuri, na hasira. Hawezi kuwa na raha kama itapita wiki bila kumtwanga makofi mkewe hata kama mkewe hana kosa, akirudi nyumbani watoto wanakimbia. Akiwa kazini utafikiri ofisi atazikwa nayo, hasira za SIMBA & YANGA anazileta hadi ofisini.
4. NYUMBU (Unafiki, uoga, na uzembe) - Wapo watu ni kama nyumbu, hata wasikie jirani yao usiku anapiga kelele za mwizi hawatoki, wanasubiri ifike asubuhi wakatoe pole. Hata wakiwa 300 wataufyata mkia kwa adui 1. Wakiwa pamoja unaweza kudhani wana ushirikiano, lakini subiri mwenzao apatwe na shida wanamkimbia kama hawamjui.
5. KENGE (Ubishi usio na maana) - Wapo watu ni kama kenge, wamekalia ubishi usio na maana. Wala hawana muda wa kuchukua tahadhari mapema, wanasubiri damu zitoke ndo wakumbuke walichoambiwa.
6. SUNGURA (Ujanja na ujuaji mwingi usio na maana, mbele giza) - Kuna watu wapo kama sungura. Hawaaminiki hata kidogo ndo maana hawapewi michongo. Wakipewa michongo ya pesa ujanja na ujuani mwingi mwisho wanaharibu kazi. Hawatulii kwenye jambo moja.

Right Marker
Dar es salaam