Kuna watu wanaamka asubuhi wakiwa hawajui leo watapata nini,

Kuna watu wanaamka asubuhi wakiwa hawajui leo watapata nini, lakini bado wanaamka na kutoka kutafuta.

Kuna anayezunguka mjini bila kazi.
Kuna anayebeba CV mfukoni kila siku.
Kuna anayesubiri simu ambayo haipigi.
Kuna aliyeanza biashara na ikafa.
Kuna aliyejaribu mara tano na bado hajapata breakthrough.

Lakini kuna kitu kimoja kinawatofautisha na walioshakata tamaa:

BADO WANATAFUTA.

Usione aibu kuanza chini.

Usione aibu kufanya kazi ambayo jana hukuwahi kufikiria kuifanya.

Usidharau 5,000 kwa sababu unaota milioni.

Usikatae kujifunza kwa sababu unaona wengine wamechelewa.

Na usikae nyumbani ukisubiri watu wakugundue.

Mtafutaji lazima ajionyeshe kwa juhudi, si kwa kulalamika.

Leo unaweza kuwa unazunguka bila kazi.

Kesho unaweza kuwa unamtafutia mwingine kazi.

Maisha yana mizunguko ambayo huwezi kuiona ukiwa bado ndani ya shida.

Kwa hiyo kama leo bado una nguvu ya kutoka, kuuliza, kujifunza, kujaribu na kuanza tena—

HUJACHELEWA.

Watafutaji wenzangu, swali la jioni ni hili:

Ni kitu gani umeamua kufanya tofauti kesho ili usiwe bado unalalamikia hali ileile baada ya mwaka mmoja?

Tuchangie uzoefu, si kejeli.
Huenda comment yako ikawa mwanzo wa mtu mwingine kusimama tena.
Ila uwe tayari kufanya kazi yoyote ili mradi mkono uende kinywani.
 
Kote umepatia.

Umekuja kukosea mwisho kabisa.

Ujaweka kile kibwagizo chako cha kuomba 20,000/= sababu una hali mbaya sana.
Screenshot_20261005-183444.jpg
 
Back
Top Bottom