Uchaguzi 2020 Kuna watu wanajua vyama vyao vikichaguliwa lazima watapata maslahi

Mkogoti

TAPELI Mkubwa
Joined
May 3, 2020
Posts
2,415
Reaction score
3,924
Habari wakuu?

Ipo hivi kelele zote hizi za upinzani sijui CHADEMA au ACT-Wazalendo pote huko kuna watu wanajua kabisa hiki chama kikiingia madarakani mmoja wapo wagombea wao akapata Urais basi lazima anajua kuna cheo lazima atapata, Muangalie mtu kama Sijui wanamwita shangazi jana anaonekana adi anacheza kwenye mkutano wa ACT-Wazalendo.

Sasa mtu kama huyo anajua lazima kama asipoteuliwa kwenye kanafasi basi ni bahati au viti maalum, Tumtazame Mdee wa CHADEMA kelele zote anajua Lissu akiingia Ikulu basi yeye uwaziri unamuhusu ndo maana anapiga kelele sana, yani wote wote ni wachumia tumbo hakuna sijui kuisaidia nini wala nini, wote ni familia zao ndo zitanemeeka lakini mtu kama mimi atanijua saa ngapi?

Na hilo neno pia linawahusu Upande ule wa kijani hakuna chochote watu tunalia na njaa matatizo chungu nzima Harafu mtu unifate eti nikapige kula kati ya CCM, ACT Wazalendo, CHADEMA nitakupiga mpaka nikuue mimi sina chama napambana mwenyewe na life langu linatosha siwezi kumpigia mtu anaenda kula hela peke ake hiyo kwangu BIG NO.


MWENYE MASIKIO NA ASIKIE πŸ€ͺπŸ€¦πŸƒ
 
Si bora hao? huyu tulienae yeye anawaangalia vyakula vyake mtaani kama ni wazuri mithili ya joketi anawapa vyeo na ni viburudisho baada ya kazi, yaani ni kwa maslahi yake binafsi πŸ€¦β€β™€οΈ πŸƒβ€β™‚οΈπŸ˜­πŸ˜­
 
si bora hao? huyu tulienae yeye anawaangalia vyakula vyake mtaani kama ni wazuri mithili ya joketi anawapa vyeo na ni viburudisho baada ya kazi, yaani ni kwa maslahi yake binafsi πŸ€¦β€β™€οΈ πŸƒβ€β™‚οΈπŸ˜­πŸ˜­
Na wewe fanya yako kwa maslahi yako...........ukombozi upo ndani yako......
 
Kwa hiyo unatakaje? kagombee wewe basi tukupigie kura.. Malalamiko yako hayana msingi kwa sababu ni lazima tuwape baadhi ya watu dhamana ya kutuongoza. Kama wataongoza kwa uadilifu au la hilo ni jambo lingine linalohitaji mjadala mpana na tofauti kabisa.

Na usipopiga kura kaa kimya no matter what... maana kama hukushiriki kuchagua basi huna uhalali wa kuhoji unavyoongozwa!
 
Siku ukijua Siasa ni maisha ndio utaamka,Hata kama ukifanya maisha yako mwenyewe, Hawa wanasiasa watakupanga namna ya kukulipisha kodi, Amka, Amka, Amka
 
Unafikiri Makonda alikuwa anatuma watu wamnyooshee bunduki Nape kwa maslahi yako?

Unafikiri akina Kabudi, Polepole na Musiba wanatoka povu kumtetea Magufuli kwa maslahi yako? Wake up buddy.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…