Kuna watu wanaleta utamaduni wa ovyo wa kutukana viongozi wa nchi. Ndugu zangu hiyo sio demokrasia

Ni vema viongozi wawe mfano bora kwa matamko yao. Maneno NONSENSE, VIDRAMA, MIKIA, SISIMIZI na zingine viachwe na Viongozi.
 
Vyovyote vile kutukana mtu yeyote sio sawa kwa maadili yetu ya Ki Afrika.
 
Hao wa kufinywa tu.

Wapite mitaa yetu halafu wamtukane wajionee.
 
Unaijua marekani wewe? Kule rais anatukanwa matusi ambayo hujawahi kuyasikia na watu wanaendelea na maisha...hapa kwetu kama kutukana ni jinai basi wapelekwe mahakamani...kama siyo jinai wataendelea kutukanwa wakifanya upumbavu...upumbavu mwingine unatakiwa kukosolewa kwa kudhalilishana, hamna namna nyingine
 
Ukijiheshimu utaheshimiwa, heshima sio hisani ni lazima! Uongozi sio umungu (divine) uongozi ni dhamana.
Unapowadharau unawaongoza na kama katiba inasema "serikali utapata madaraka yake kutoka kwa wananchi" Tafsiri yake ni kwamba viongozi wa serikali sio miungu ni watumishi wa wanannchi, wanaishi kwa kulipwa mishahara itokano na Kodi za wananchi bila kujali dini, tangi, jinsia, chama au hadhi ya mtu.
Kwa msingi huo ni kwamba uongozi ni "dhamana" hivyo basi qnayepewa nafasi ya uongozi sio kwamba ana akili sana au helima sana au anakua sana no! Ni amepewa "dhamana" kwa niaba ya wengine wote. Hivyo anapaswa kulinda dhamana hiyo kwa kuwa mwadilifu wakati wote na mtu wa Haki kwa wakati wote.

Tanzania ni nchi ya kidemokrasia inayojengwa katika misingi ya utawala Bora, utawala wa Sheria, Haki za binadamu, vyama vingi, uhuru wa kukusanyika, uhuru wa kutoa na kupokea habari, uhuru wa kujieleza na uhuru wa kutoa fikra zako au mawazo Yako. Yote haya yanafanyika kwa muongozo wa Sheria (legal framework) na hiyo imetokana na Sheria tulizokubaliana kwa pamoja kama taifa nazo msingi wake ni katiba. Kiongozi yeyote anayekua madarakani kwa namna ya kuchaguliwa au kuteuliwa au kwa namna yoyote Ile ana wajibu katika kiapo chake kuilinda, kuiheshimu na kumtetea katiba ambayo ni Sheria mama.
Tatizo linakuja kwamba viongozi hao wanapokwenda kinyume hadharani hawataki kukosolewa hadharani.

Kwa mantiki hiyo wameamua kujitwalia Sheria mikononi ikiwemo kutwaa uhai wa wakosoaji na kuwanyima Haki ya kuishi ambayo wameapa kuilinda kwa kupitia katiba.

Kwakua nchi hii inazingatia misingi ya Sheria na uwajibikaji kwa wananchi na viongozi, ingekua vyema kabisa watu mnaosema kwamba wanawatukana viongozi mngewapeleka mahakamani ikathibitika bayana pasina shaka wametuka na wakakabiliana na adhabu.
Tukiwaambia mlete kesi hata tatu amabazo mmewashitaki watu kwa kuwatukana viongozi hakuna hata Moja. Kwa maana hiyo hamjui nchi Ina utawala wa Sheria?

Hii inaleta picha kwamba mnapokoaolewa mnatafuta huruma kwamba viongozi wanatukanwa. Huu ni ujinga wa kiwango Cha lami. Kama kiongozi ni mzembe aambiwe ni mzembe. Tatizo ni kwamba wajinga wamekua wengi na miongoni mwao wamepatikana viongozi wajinga vile vile.

Na sifa mojawapo ya kiongozi mjinga ni kukataa kukosolewa na kujirekebisha. Ukosoaji unapozidi huamua kutumia nguvu ikiwemo kupiga au kujua Ili ujinga wake usiwe bayana na aogopwe. Na mara kadhaa kuamini Kila anachoambiwa.
Mwalimu aliandika kitabu "tujisahihishe"
Lucas Mwashambwa
 
Watu wanakosoa lakini ninyi mnasema ni matusi.

Kiongozi anawaita raia wake mbwa, wana mikia, samaki na kadhalika. Nenda kamkanye.

Utamaduni wa kukosoa ni pigo kubwa kwa chama cha majambazi
 
Naunga mkono hoja,kutukana viongozi, kutoa lugha chafu na kuwasingizia mambo ambayo hawajayafanya kisa tu uichafue serikali ni tabia za kishenzi na hazifai katika nchi yetu.

Viongozi wa upinzani kosoa kwa lugha ya staha na sisi wanachi tunaelewa vizuri tu huna haja ya kutoa matusi wala kudanganya ili serikali ichafuke.
 
Wametukana, wamesema nini? Wametukana lini? Wametoa matusi gani? Umerukia kwenye conclusion bila kuweka wazi hoja yako. Unataka tujadili conclusion? Hoja hapa JF haitakiwi kuletwa kama mahubiri ambapo wote yabidi tuitikie, Amin.
 
Hakuna tusi baya kama kwa mtawala kuruhusu vyombo vya dola kuteka na kuua watu eti kwa vile wanakukosoa. Halafu wakilalamika kuwa ndugu zao wanatekwa, unasema eti ni drama. Wakilalamika kuwa ndugu zao wanauawa na vyombo vya dola, ukawaambia kuwa eti kifo ni kifo, kote Duniani watu wanauawa. Haya ni matusi na kejeli mbaya kupindukia kuliko tusi lolote ambalo mdomo wa mwanadamu unaweza kutamka..

Yeyote asiyethamini uhai wa binadamu wenzake kama ulivyo wa kwake, ni hayawani. Heshima ya kwanza, tuupe thamani uhai wa kila mwanadamu. Hii ndiyo heshima kuu ambayo inaweza kurudisha heshima kwa viongozi.
 
Una uhakika Marekani unayoizungumzia ni hii wengine tunayoifahamu au ni marekani nyingine!
 

Watakwambia, mbona marekani wanawatukana matusi ya mwilini kabisa na si ya nguoni.
 
Ila viongozi hao hao kuwaambia Wananchi sisi ndo mabosi wao kwamba Tumeota mikia nisawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…