Kuna watu wanaumwa magonjwa ya tumbo/Kipindupindu maeneo tofauti ya Tunduma, lakini sijasikia tamko la Serikali

Kuna watu wanaumwa magonjwa ya tumbo/Kipindupindu maeneo tofauti ya Tunduma, lakini sijasikia tamko la Serikali

Kayugumis

Senior Member
Joined
Jun 6, 2022
Posts
107
Reaction score
97
Huku kwetu Tunduma karibu maeneo yote kuna changamoto ya watu kuumwa magonjwa ya tumbo na wengine kipindupindu lakini hatusikii mamlaka zikiweka wazi kuhusu suala hilo hadharani.

Kumekuwa na taarifa kuwa kuna watu wanapoteza maisha kwa maambukizi ya tumbo na kadhaa tunashuhudia Wataalamu wa Afya wanahusika kwenda kuzika wapendwa wetu ikiwemo katika kata ya Mpemba lakini bado haiwekwi wazi nini kinaendelea.

Tunatamani Watu wa Afya wafanye uchunguzi na kutoa tahadhari maana hali ni mbaya, kama kuna mlipuko wowote iwe ni Kipindupindu au ugonjwa mwingine wowote watuambie mapema ili tuwe makini.

Pia soma ~ Songwe: Mganga Mkuu wa Mkoa afafanua madai ya kusambaa kwa magonjwa ya tumbo na kipindupindu
 
Back
Top Bottom