Kuna watu wapo kwenye taasisi lakini wanashindwa kujitambua

changaule

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2020
Posts
6,039
Reaction score
10,151
Habari wadau wa michezo,

Jana kulifanyika mchezo kati ya Yanga vs Singida big stars. Ni mechi ambayo Yanga wameibuka ushindi mnono. Mazingira ya hii watu wengi wamehoji juu ya aina soka walilocheza Singida Big Stars kuwa ni kiwango cha chini hivyo wengi wakihusisha juu ya maagizo toka juu. Hilo sio mada yangu na naomba nisilizungumzie sana hilo kwasababu zinatumika hisia zaidi.

Naomba niende kwenye mada sasa, mtu umeajiliwa Yanga lakini unafanya matukio ambayo sio professional kabisa na ambayo moja kwa moja yanaleta taharuki kwa wapenzi wa soka una maana gani kama sio kuharibu taswira ya timu?

Binafsi sioni mantiki yoyote ya kiongozi kutoka timu ya Yanga kupiga picha na wachezaji wanaoimbwa ndani ya Singida big stars tena kuelekea kwenye mchezo unaofuta dhidi yao. Je unawasilisha ujumbe gani mbele ya wapenda soka? Mantiki ya kufanya vile ni nini kama sio kuharibu taswira ya Yanga ili kila mtu awaze tofauti kuhusu wapinzani hao wa Yanga? Huu ni utoto sio uweledi katika kazi. Iwe Yanga imenunua mechi basi wewe umehusika kuihabarisha wapenda soka na pia kama Yanga haikuhusika na ununuaji wa mechi basi wewe umehusika kuitengenezea Yanga taharuki na kuichafua Yanga. Ulichokifanya sio kama ni mtoto haujitambui ila umekusudia kufanya hivyo kwa lengo lako maalumu.

Jambo lingine ambalo limekuja kuniacha hoi ni Admin wa Singida big stars kaja kupost hii picha kwenye official page ya timu halafu kibaya zaidi wakati mechi inaendelea kaja kupost taharuki nyingine tena kuwa hata yeye admin ana wasiwasi kuna Trab na Trat. Ni kauli ambayo naye akiwa na mashaka na Taasisi ambayo anaifanyia kazi kuwa huenda kuna namna imefanyika. Unapofanya kazi taasisi mjifunze kutosababisha taharuki.
IMG_20221118_122424.jpg

Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app
 
Mkuu umeandika Uzi mrefu lakini umeshindwa kufanya utafiti na kujua hii picha ilipigwa lini?

Hii picha sio ya jana maana mi niliiona imepostiwa toka siku singida anachezq na azam sasa wewe kwa kukurupuka kwako unaundia hoja kitu ambacho hujui kimetokea lini?
 
Mkuu ungefanya Kwanza utafiti kujua hii picha ilipigwa lini, ni ya muda mrefu Sana kipindi Singida wapo DAR wanacheza na Azam tena hao jamaa walipewa shavu la kutangaza bidhaa za GSM pale dukani kwake ndo hizo picha zilipigwa
 
Mkuu umeandika Uzi mrefu lakini umeshindwa kufanya utafiti na kujua hii picha ilipigwa lini?

Hii picha sio ya jana maana mi niliiona imepostiwa toka siku singida anachezq na azam sasa wewe kwa kukurupuka kwako unaundia hoja kitu ambacho hujui kimetokea lini?
Msamehe Bure. Ni pure type ya wabongo. Kujifanya ujuaji mwingiiiiiiii kumbe hakuna kitu

Baada ya mechi ya Jana kila mtu anajifanya mchambuzi wa soka hususani la Yanga

Baada ya ajali ya Precision kila mtu alijifanya mchambuzi wa ndege

Ujinga mtupu
 
Watu wajinga wajinga kama Hawa ndo wanafanya mashabiki waonekane hawajielewi.
 
Sawa tumekupata Singida kauza mechi kwa Yanga. Mbona Simba ilivonunua kwa Mtibwa hujasema. Mbona Simba ilivouza kwa Azam hujasema.

Mbona Simba ilivyouza mechi kwa Yanga kwenye FA na ngao ya hisani hujasema. Lakini situmeshakubaliana kila timu ishinde mechi zake
 
Mkuu umeandika Uzi mrefu lakini umeshindwa kufanya utafiti na kujua hii picha ilipigwa lini?

Hii picha sio ya jana maana mi niliiona imepostiwa toka siku singida anachezq na azam sasa wewe kwa kukurupuka kwako unaundia hoja kitu ambacho hujui kimetokea lini?
Bnafsi hilo sikujua nimeona ndio reference kubwa inayotumika mitandaoni jana na leo nikajua imetoka jana hiyo picha.

Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app
 
Mkuu umeandika Uzi mrefu lakini umeshindwa kufanya utafiti na kujua hii picha ilipigwa lini?

Hii picha sio ya jana maana mi niliiona imepostiwa toka siku singida anachezq na azam sasa wewe kwa kukurupuka kwako unaundia hoja kitu ambacho hujui kimetokea lini?
Sikujua hilo, kama ipo hivyo basi kuitumia hiyo picha kwa matumizi ya matokeo ya jana ni upuuzi.

Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app
 
Bnafsi hilo sikujua nimeona ndio reference kubwa inayotumika mitandaoni jana na leo nikajua imetoka jana hiyo picha.

Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app
Simamia ulichoandika wasikutoe kwenye mstari..haijalishi picha ilipigwa lini(kama picha ya muda mrefu kwanini iwekwe kwenye ukurasa wao jana?)..uko sahihi na hoja zako.
 
Sasa kama hukujua, si ungenyamaza kimya! Kelele za nini, kiasi cha kufikia kumuambia mtu ana akili za kitoto! Kumbe mwenye hizo akili za kitoto ni wewe mwenyewe!

Halafu unaelewa maana pana ya neno michezo? Michezo ni furaha, michezo ni urafiki, michezo ni afya, michezo ni ajira, michezo ni burudani! Na wala siyo uadui , au vita kama unavyotaka kuwaaminisha watu.

Yaani kwa sababu Ali Kamwe ni Meneja Habari wa Yanga, basi haruhusiwi kupiga picha za ukumbusho na wachezaji wa Singida Big Stars!! Na ikitokea akafanya hivyo, basi mechi imeuzwa!!

Ifikie wakati Watanzania tubadilike. Hizi akili za matope sasa ni too much.
 
Sikujua hilo, kama ipo hivyo basi kuitumia hiyo picha kwa matumizi ya matokeo ya jana ni upuuzi.

Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app
Ndo maana nimekwambia uwe unafwatilia jambo kabla hujaliandika.
Maana kuna wajinga wengi huwa wana crop picha kuficha ni ya lini Ili aweke maneno yake ionekane kweli.
Na watanzania hatunaga kufwatilia basi tunakurupuka nalo.
 
Simamia ulichoandika wasikutoe kwenye mstari..haijalishi picha ilipigwa lini(kama picha ya muda mrefu kwanini iwekwe kwenye ukurasa wao jana?)..uko sahihi na hoja zako.
Acheni uzwazwa basi. Asimamie alichoandika kuwa Jana kiongozi wa Yanga kapiga picha na wachezaji wa Singida
 
Shukran nyingi ziende kwa waziri Madelu kwa kuwawekea Uto timu ya kuvuna jumla ya point 6 kwenye ligi.
 
Sawa tumekupata Singida kauza mechi kwa Yanga. Mbona Simba ilivonunua kwa Mtibwa hujasema. Mbona Simba ilivouza kwa Azam hujasema. Mbona Simba ilivyouza mechi kwa Yanga kwenye FA na ngao ya hisani hujasema. Lakini situmeshakubaliana kila timu ishinde mechi zake
Simba tu ndio wenye uhalali wa kufungwa na Yanga wengine wote hua wanahongwa
 
Sasa kama hukujua, si ungenyamaza kimya! Kelele za nini, kiasi cha kufikia kumuambia mtu ana akili za kitoto! Kumbe mwenye hizo akili za kitoto ni wewe mwenyewe!

Halafu unaelewa maana pana ya neno michezo? Michezo ni furaha, michezo ni urafiki, michezo ni afya, michezo ni ajira, michezo ni burudani! Na wala siyo uadui , au vita kama unavyotaka kuwaaminisha watu.

Yaani kwa sababu Ali Kamwe ni Meneja Habari wa Yanga, basi haruhusiwi kupiga picha za ukumbusho na wachezaji wa Singida Big Stars!! Na ikitokea akafanya hivyo, basi mechi imeuzwa!!

Ifikie wakati Watanzania tubadilike. Hizi akili za matope sasa ni too much.
Haya ndio yale ya Haji Manara kipindi yupo huko mikiani Senzo alienda kumsalimia ndugu zake Kaizer Chiefs akaropoka eti kaenda kuwapa mbinu waifunge Simba ujinga mtupu
 
Sasa kama hukujua, si ungenyamaza kimya! Kelele za nini, kiasi cha kufikia kumuambia mtu ana akili za kitoto! Kumbe mwenye hizo akili za kitoto ni wewe mwenyewe!

Halafu unaelewa maana pana ya neno michezo? Michezo ni furaha, michezo ni urafiki, michezo ni afya, michezo ni ajira, michezo ni burudani! Na wala siyo uadui , au vita kama unavyotaka kuwaaminisha watu.

Yaani kwa sababu Ali Kamwe ni Meneja Habari wa Yanga, basi haruhusiwi kupiga picha za ukumbusho na wachezaji wa Singida Big Stars!! Na ikitokea akafanya hivyo, basi mechi imeuzwa!!

Ifikie wakati Watanzania tubadilike. Hizi akili za matope sasa ni too much.
Wapi nimeandika kuwa ni vita? Nilichoongelea ni swala la uweledi kwenye kazi za taasisi ili kutoleta taharuki. Picha ilipigwa siku nyingi haiku trend lakini Admin wa Singida big stars anakuja kui post kwenye official page ya timu ya Singida anatuma ujumbe gani? Admin kuandika nina wasiwasi kuna Trab na Trab anawasilisha jambo gani?
Timu ya Singida big stars tayari tokea awali ilishavuja kiongozi wake ni mtu halafu bado mazingira ya taharuki yanafanyika ili watu waelewe zaidi.

Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app
 
Ila wabongo mna shida sana. Mbona simba akifungwa na yanga hatusikii haya? Hua tunaambiwa kwamba Yanga yeye mafanikio yake ni kuifunga simba na kimataifa haiwezi.
Ni kwa nn tusisimamie hiyo kauli kwa upande wa pili kwamba yanga yeye mafanikio yake ni kuzifunga timu za ndani tu na ikktoka nje inafungwa?
Maana kama mkubwa anapigwa, iweje amtegemee mdogo kumpiga aliempiga mkubwa?
 
Habari wadau wa michezo.
Jana kulifanyika mchezo kati ya Yanga vs Singida big stars. Ni mechi ambayo Yanga wameibuka ushindi mnono. Mazingira ya hii watu wengi wamehoji juu ya aina soka walilocheza Singida big stars kuwa ni kiwango cha chini hivyo wengi wakihusisha juu ya maagizo toka juu. Hilo sio mada yangu na naomba nisilizungumzie sana hilo kwasababu zinatumika hisia zaidi.

Naomba niende kwenye mada sasa, mtu umeajiliwa Yanga lakini unafanya matukio ambayo sio professional kabisa na ambayo moja kwa moja yanaleta taharuki kwa wapenzi wa soka una maana gani kama sio kuharibu taswira ya timu?

Binafsi sioni mantiki yoyote ya kiongozi kutoka timu ya Yanga kupiga picha na wachezaji wanaoimbwa ndani ya Singida big stars tena kuelekea kwenye mchezo unaofuta dhidi yao. Je unawasilisha ujumbe gani mbele ya wapenda soka? Mantiki ya kufanya vile ni nini kama sio kuharibu taswira ya Yanga ili kila mtu awaze tofauti kuhusu wapinzani hao wa Yanga? Huu ni utoto sio uweledi katika kazi. Iwe Yanga imenunua mechi basi wewe umehusika kuihabarisha wapenda soka na pia kama Yanga haikuhusika na ununuaji wa mechi basi wewe umehusika kuitengenezea Yanga taharuki na kuichafua Yanga. Ulichokifanya sio kama ni mtoto haujitambui ila umekusudia kufanya hivyo kwa lengo lako maalumu.

Jambo lingine ambalo limekuja kuniacha hoi ni Admin wa Singida big stars kaja kupost hii picha kwenye official page ya timu halafu kibaya zaidi wakati mechi inaendelea kaja kupost taharuki nyingine tena kuwa hata yeye admin ana wasiwasi kuna Trab na Trat. Ni kauli ambayo naye akiwa na mashaka na Taasisi ambayo anaifanyia kazi kuwa huenda kuna namna imefanyika. Unapofanya kazi taasisi mjifunze kutosababisha taharuki.View attachment 2420162

Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app

Watz tunachanganya mpira na siasa
Ulaya wenzetu wachezaji ama viongozi kupiga picha na wachezaji wa timu pinzan ni k2 cha kawaida
Wachezaji wa Maccabi Haifa walibook jezi ya Mess kbl hata ya Mechi
 
Back
Top Bottom