changaule
JF-Expert Member
- Jan 10, 2020
- 6,039
- 10,151
Habari wadau wa michezo,
Jana kulifanyika mchezo kati ya Yanga vs Singida big stars. Ni mechi ambayo Yanga wameibuka ushindi mnono. Mazingira ya hii watu wengi wamehoji juu ya aina soka walilocheza Singida Big Stars kuwa ni kiwango cha chini hivyo wengi wakihusisha juu ya maagizo toka juu. Hilo sio mada yangu na naomba nisilizungumzie sana hilo kwasababu zinatumika hisia zaidi.
Naomba niende kwenye mada sasa, mtu umeajiliwa Yanga lakini unafanya matukio ambayo sio professional kabisa na ambayo moja kwa moja yanaleta taharuki kwa wapenzi wa soka una maana gani kama sio kuharibu taswira ya timu?
Binafsi sioni mantiki yoyote ya kiongozi kutoka timu ya Yanga kupiga picha na wachezaji wanaoimbwa ndani ya Singida big stars tena kuelekea kwenye mchezo unaofuta dhidi yao. Je unawasilisha ujumbe gani mbele ya wapenda soka? Mantiki ya kufanya vile ni nini kama sio kuharibu taswira ya Yanga ili kila mtu awaze tofauti kuhusu wapinzani hao wa Yanga? Huu ni utoto sio uweledi katika kazi. Iwe Yanga imenunua mechi basi wewe umehusika kuihabarisha wapenda soka na pia kama Yanga haikuhusika na ununuaji wa mechi basi wewe umehusika kuitengenezea Yanga taharuki na kuichafua Yanga. Ulichokifanya sio kama ni mtoto haujitambui ila umekusudia kufanya hivyo kwa lengo lako maalumu.
Jambo lingine ambalo limekuja kuniacha hoi ni Admin wa Singida big stars kaja kupost hii picha kwenye official page ya timu halafu kibaya zaidi wakati mechi inaendelea kaja kupost taharuki nyingine tena kuwa hata yeye admin ana wasiwasi kuna Trab na Trat. Ni kauli ambayo naye akiwa na mashaka na Taasisi ambayo anaifanyia kazi kuwa huenda kuna namna imefanyika. Unapofanya kazi taasisi mjifunze kutosababisha taharuki.
Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app