John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 379
- 1,412
Picha: world-heart-federation.org
Magonjwa hayo pia yamekuwa yakichangia wahusika kukumbwa na magonjwa mengine mbalimbali kwa kuwa moyo ni injili ya ufanisi wote wa binadamu.
Nimepata nafasi ya kuwasikiliza wataalam wa afya kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete mnamo Septemba 29, 2025, nikaona ni busara nichanganue ujumbe walioutoa katika lugha nyepesi ili Dunia ikumbushwe umuhimu wa kujali afya zao na kutambua japo elimu ndogo ya magonjwa ya moyo.
Wataalam hao ambao wote ni Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo ni;
1. Mkurugenzi wa JKCI, Dkt. Peter *******
2. Eva Wakuganda, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto wa JKCI - Dar Group
3. Mkurugenzi wa JKCI - Dar Group, Dkt. Tulizo Shemu.
Naamini ukimaliza kusoma article hii utakuwa umepata kitu fulani kuhusu afya yako au ya mpendwa wako…
Magonjwa ya Moyo yanapoteza Watu Milioni 20 kwa Mwaka Duniani
Dkt. Peter *******: Magonjwa ya moyo yanazidi kuongezeka kwa kasi Duniani, takwimu zinaonesha kuwa takribani Watu Milioni 20 wanapoteza maisha kutokana na magonjwa ya moyo kila mwaka.
Kusoma Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zipo hapa ~An estimated 19.8 million people died from CVDs in 2022
Global trends in number of deaths due to cardiovascular diseases, 1990-2019.
Mkurugenzi wa JKCI, Dkt. Peter *******
Ameongeza kuwa haishauriwi kula vyakula vya wanga na vyenye mafuta mengi, kupunguza kula kwa wingi vyakula vyenye protini nyingi mfano nyama za Wanyama wanaonyonyesha kama vile mbuzi, kondoo, ng’ombe pia ni muhimu kuzingatia kufanya mazoezi.
Magonjwa nyemelezi na shinikizo la damu yanachangia sana watu kupata magonjwa ya moyo.
Hivyo, ni vizuri kuhakikisha angalau unafanya mazoezi kwa nusu saa hata mara tatu kwa wiki, itakusaidia kulinda moyo wako.
Pia, ni muhimu kufahamu kuhusu uzito, presha, uzito, sukari na kerosto yako ya damu. Hiyo itakusaidia kujua jinsi ya kudhibiti mwili wako.
Unaweza kuishi na Ugonjwa wa moyo muda mrefu bila kujua
Dkt. Eva Wakuganda: Magonjwa ya moyo yanaweza kuwa kimya kwa muda mrefu, yanaweza kumuanza mtu akiwa mdogo na kwenda nayo hadi anapokuwa mtu mzima pasipo mhusika kutambua.
Hivyo ni vizuri kuwa na kawaida ya kupima afya mara kwa mara kuangalia afya ili kama kuna tatizo uliwahi mapema na lipate matibabu mapema pia.
Eva Wakuganda, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto wa JKCI - Dar Group
Upande wa Watoto wengi wao wanapopata shida ya masuala ya moyo ni vizuri kupatiwa matibabu mapema kwa faida ya afya ya mtoto husika.
Matatizo ya moyo kwa Watoto yanaweza kuanza kwa wahusika kuzaliwa mfano kuzaliwa na tundu katika moyo au kuzaliwa na mshipa mmoja wa moyo haupo au umebana.
Pia, Watoto wanaweza kupata matatizo ya moyo hata baada ya kuzaliwa, mfano wanaweza kupata bakteria wanaoenda kukaa kwenye mlango wa moyo na kuathiri au wanaweza kupata matatizo ya kwenye koo kisha wale bakteria wakasababisha mwili uka-react ukatengeneza kinga ambazo zimejipiga zenyewe na kutengeneza kinga ambazo zimejipiga zenyewe.
Baadhi ya Dalili za Ugonjwa wa Moyo kwa mtoto
Mtoto kutokwa na jasho jingi mara kwa mara, anachoka sana, analalamika mapigo ya moyo yanaenda mbio…
Sababu za mtoto kuzaliwa na tatizo la Moyo
Zipo nyingi, mfano mjamzito akiwa na tatizo la Kisukari ambalo linachangia mara nne zaidi magonjwa kwa Mtoto tumboni.
Ni muhimu mjamzito afanye maandalizi kabla au mara tu anapopata ujauzito kwa kufika kliniki na kupata muongozo na kufanya vipimo.
Uvutaji wa Bangi, Tumbaku, Pombe kwa Mjamzito ni hatari
Mjamzito akiwa anatumia kwa wingi uvutaji wa bangi, sigara, pombe n.k vinachangia kuathiri ukuaji wa mtoto, pia mjamzito anapopata magonjwa makali.
Pia, matumizi ya baadhi ya dawa yanaweza kuchangia, mfano dawa za presha, shinikizo la juu la damu au kifafa zinaweza kuathiri uumbaji wa mtoto katika miezi mitatu ya kwanza, hivyo mjamzito hatakiwi kutumia dawa bila maelekezo zipo baadhi zinaweza kuwa na athari kwa mtoto.
Sababu nyingine ni kama kwenye familia kuna mtu ana magonjwa ya moyo kuna ‘risk’ mara mbili zaidi ya kupata ugonjwa wa moyo pia kwa mtoto.
Umri wa mama unaweza kuwa sababu
Mjamzito anapokuwa na umri wa miaka 35 au 40 au zaidi anakuwa na ‘risk’ ya kusababisha mtoto kuzaliwa na changamoto ya moyo, hivyo ndivyo ilivyo kwa mjamzito anapokuwa na umri mdogo mfano miaka 15 au chini ya hapo pia ni hatarishi kwa mtoto.
Mjamzito kutokula vizuri
Vyakula ambavyo havina folic Asid vinaweza kuchangia kupata mtoto mwenye shida ya moto.
Asilimia 60 hawajui kama wana maradhi ya moyo
Dkt. Tulizo Shemu: Sababu nyingi za magonjwa ya moyo na nyingi zinatokana na mfumo wa maisha, uelewa wa maradhi ya moyo unaweza kusaidia kupunguza magonjwa ya moyo.
Takwimu za kitaalam za Kidunia zinaonesha zaidi ya 60% ya watu wenye maradhi ya moyo wamekuwa wakiishi nayo pasipokuwa na taarifa juu magonjwa yanayowasumbua.
Watu wengi walioshindwa kudhibiti maradhi ya moyo wamejikuta wakipata maradhi mengine ikiwemo kufikia hatua ya kusafisha figo, jambo ambalo ni gharama kubwa na ni ngumu kumudu hasa kwa maisha ya Watanzania wengi.
Mkurugenzi wa JKCI - Dar Group, Dkt. Tulizo Shemu
Kuzibua mshipa mmoja wa moyo inaweza kugharimu hadi Shilingi milioni 6, kufunga kifaa cha umeme wa moyo ni Shilingi Milioni 10 na moyo ukishindwa kabisa kufanya kazi unatakiwa kufungwa kifaa kinachogharimu Shilingi Milioni 30.
Zamani zile shida za kiafya ambazo zilikuwa zinawapata Wazee sasa hivi zinawapata vijana, hiyo ni kutokana na mfumo wa maisha ya sasa. Tupunguze vyakula vya kwenye makopo, tule vyakula vya asili kwa wingi, tupunguze nyama nyekundu, kupunguza matumizi ya tumbaku na tufanye mazoezi.
Dalili za shinikizo la damu
Watu wanaofika JKCI wakisumbuliwa na magonjwa ya moyo kati yao zaidi ya 70% wanasumbuliwa na Shinikizo la Damu.
Dalili za Shinikizo la Damu ni kusikia uchovu usiokuwa na sababu, kichwa kuuma, moyo kwenda haraka zaidi ya kawaida, macho kutoona vizuri na kuwa na ukungu, kiharusi, miguu kuvimba na kushindwa kupumua vizuri.
Pia soma:
~ Dkt. *******: Wastani wa Watoto 10,000 huzaliwa nchini wakiwa na matatizo ya moyo kila mwaka
~ Je moyo wako upo salama? Fahamu kuhusu heart failure (kushindwa kwa moyo)