Kuna watu...

Kuna watu...

Dr Lizzy

Platinum Member
Joined
May 25, 2009
Posts
31,009
Reaction score
60,629
....wana roho mbaya sana!!Wanamfanya mtu aamini ni marafiki wa kweli....wanaaminiwa na kuTREATwa kwa heshima na mapenzi kama marafiki alafu wanageuka na kumfanyia mwenzao kitu ambacho rafiki hawezi kufanya hata siku moja.Hata adui tu ataona aibu kidogo. Binafsi nimekua na bahati (mbaya) sana ya kukutana na watu wa aina hii....nadhani ntaanza kuhitaji watu waniombe urafiki kama. wanavyoomba uchumba na nichukue zaidi ya mwaka kuwachunguza na kujua ni watu wa aina gani kabla ya kuwapa sifa na cheo cha urafiki kwenye maisha yangu!!Kama na wewe uko hivi badilika maana sidhani kama mnapata faida yotote.
 
....wana roho mbaya sana!!Wanamfanya mtu aamini ni marafiki wa kweli....wanaaminiwa na kuTREATwa kwa heshima na mapenzi kama marafiki alafu wanageuka na kumfanyia mwenzao kitu ambacho rafiki hawezi kufanya hata siku moja.

Ni kweli Lizzy..lakini kumbuka kuna aina mbili za hawa watu. Aina ya kwanza ni wale watu wenye kujifanya wana nia njema hapo mwanzo lakini kwa malengo maalum. Aina hii mara nyingi inasukumwa na tamaa binafsi hasa kwa wanaume. Jinsi ya kuwaepuka watu hawa ni kufungua roho yako half way..huku upande wa pili kukiwa na kufuli la nguvu....Haina haja ya mtu kumwambia Background yako yote..ongea nae lile la kawaida na funga mlango...marafiki wa aina hii mara nyingi wanakosa subira kwa kile wanachotaka..mwisho upotea taratibu. Lakini ..becareful...kuna wachache Vin'gan'ganizi...hawa wanakuwa na subira tena hawa ni wabaya sana kwani ni vigumu kuwajua.

Kundi la pili ni wale ambao toka mwanzo wamepania kukumaliza.. Ni rahisi sana kuwajua watu hawa kwani upendo wao unaonekana dhahiri ni wa kinafki ..hebu fikiri mtu mnachat anakuPM ..kesho anakutumia zawadi na kukuhahidi kukusadia mambo kadhaa. Njia pekee ya kuwaepuka watu wa aina hii ni kuwapa tabasamu la mdomoni lakini moyoni kuna kufuli la nguvu...

All in all, We don't lose friends, but we control them!

Binafsi nimekua na bahati (mbaya) sana ya kukutana na watu wa aina hii....

Ni vizuri kama umegundua hilo kwani umeshafaulu mtihani..Nawapa pole wale vijana wenzetu ambao bado hawajagundua hili..
 
My life rule: do not trust anyone, and expect anything stupid n funny from anyone,ukifanya hv mama hata m2 afanye nn hamna kitakachokushtua,
 
Pole sana Lizzy,ukweli unaweza ukawa na frinds weeeengi lkn mmoja tu au wawili ndo akawa na urafiki wa kweli!usiwe una disclose kirahisi pia kuwa neutral...
 
Shangazi,kiuhalisia hakuna kitu kama urafiki,urafiki umeumiza wengi hata mimi nikiwa mmoja wa wahanga wa hiki kitu urafiki,nimejifunza kuwa sina rafiki wala adui nawapenda wote kwa usawa,.Bob Marley aliwahi kusema;Love is the only force capable of transforming an enemy to a friend!
 
wamekufanyaje dadangu.... Pole najua huko Ungalimited wengi wao wanakuwa wametoka Mererani au Loliondo...wasamehe uanze upya..
 
Binadamu ni mnyama asiyetabilika,vivyo vema kumchukulia kila mtu kama halivyo na kuishi naye kwa taadhari kubwa!!
 
....wana roho mbaya sana!!Wanamfanya mtu aamini ni marafiki wa kweli....wanaaminiwa na kuTREATwa kwa heshima na mapenzi kama marafiki alafu wanageuka na kumfanyia mwenzao kitu ambacho rafiki hawezi kufanya hata siku moja.Hata adui tu ataona aibu kidogo. Binafsi nimekua na bahati (mbaya) sana ya kukutana na watu wa aina hii....nadhani ntaanza kuhitaji watu waniombe urafiki kama. wanavyoomba uchumba na nichukue zaidi ya mwaka kuwachunguza na kujua ni watu wa aina gani kabla ya kuwapa sifa na cheo cha urafiki kwenye maisha yangu!!Kama na wewe uko hivi badilika maana sidhani kama mnapata faida yotote.

...pole Lizzy, lick your wounds and move on!...

haupo peke yako, wengi tumepitia huko...Marafiki wengi ni wanafiki. Trust your instincts!
Unapotendwa mara mbili tatu na marafiki zako chukulia nawe ni sehemu ya tatizo...usiwaamini 100%.
 
.... Binafsi nimekua na bahati (mbaya) sana ya kukutana na watu wa aina hii....

Aisee!
Pole sana,
Labda jaribu kuwa reserved kwa kiwango fulani. Jenga urafiki na watu kwa machale.
 
Kuna watu na viatu, jaribu kuwatofautisha wala hawatakupa shida
 
do not trust anybody but yourself
urafiki uwepo lakini kwa mipaka
hakuna adui mbaya kama aliyekuwa rafiki yako
 
aaah...sio watu wa kuwaamini na kuwashirikisha mambo yako ya ndani sana ya maisha.hata kama akiwa ni mmoja iko siku atakujeuka tuu.tuwe na marifiki lakin kuwa na mipaka. marifiki wengine wabaya kuliko hata maadui..adui hakujui kiundani..rafiki wa karibu yes..maana rafiki mwingine unakuwa karibu kiasi kwamba mna-share mambo mengi ya maisha..happy and unhappy issues....then anakuwa ameshakufahamu ana-take advantage..siku atakuvua nguo hadharani hutaamini. imeshanikumba...POLE SANA LIZZY
 
Lizzy Kuna watu na viatu.



weeke end njema just enjoy your life




teh teh teh teh
 
Last edited by a moderator:
Good Friends are like Stars......, You dont Always See them, But You Always Know they are There....

Just as I know you are There..... Lizzy!!!

Na kama marafiki zetu wametukosea ni bora tukiwasamehe..., hapo sisi ndio tutakuwa True Friends Kwao, kuliko na sisi tukiwatupa basi tutakuwa hatuna tofauti na wao....
 
Pole dada.. siku nyingine usiamini sana rafiki/marafiki.. Ni binadamu kama wengine, na wana mapungufu yao kama binadamu wengine. Usidisclose kila kitu chako kwa rafiki yako hata kama una mwamini vipi.
 
binadamu wengine ni wabaya/hatari heri wanyama pori. wanajifunika ngozi ya kondoo na ndani ni mbwa wa mwituni kabisa. rafiki mnafiki hana tofauti na muuaji.

Do not trust people until your are satisfied enough with the reason they give you to trust them. mijitu mingine ni BS! Heri kufanya urafiki na mbwa abweke nje usiku kuliko binadamu mnafiki.
 
hiyo inatokea sana, tukiwemo wengii tulio patikana na matatizo kama hayo,, pole mpenzi, ndio maisha,
 
Back
Top Bottom