Kuna wengine hatujui tulipokosea

Dadakidoti

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2024
Posts
399
Reaction score
1,409
Nimesoma kisa cha patrickk na bado nafuatilia wakati tukiendelea kumsubiria naomba nami nishare na nyinyi historia ya maisha yangu kwa ufupi. nia visa humu ni kujifunza, kushauriana na kutiana moyo. Karibu.

Kwa jina naitwa Lisa (sio jina halisi) natokea katika mmoja wa mikoa ya kanda ya ziwa.

Nilipoanza kujitambua kuwa mimi ni nani nilikuwa nikiishi kijijini kwa babu na bibi wazaa baba. Wazazi wangu hawakuwa pale walikuwa mjini. Jinsi navyoeendelea kukua ndo nagundua kuwa hawapo pamoja wametalikiana. Mama yupo na Maisha yake na baba pia yupo na mke mwingine na wana Watoto.

Niliendelea kukua nikapelekwa shule ya msingi huko kijijini. Nikaendelea na masomo yangu kama kawaida darasani nilikuwa na akili sana hali iliyonipelekea kuwa kipenzi cha walimu. Mpaka nafika darasa la nne nilikuwa sijawahi kuziona sura za wazazi wangu wala wadogo zangu ambao nawasikia kwa majina tu.

Nakumbuka nilikuwa nje tupo likizo tunajiaanda kuingia darasa la tano nilikuwa nje naosha vyombo mara wakaja watu wa baiskeli ndo tuseme walikuwa ndo bodaboda wa kipindi kile. Na mizigo mabegi ya kutosha na mmababa mmoja hivi nikamwamkia akaniangalia sana akaanza kulia sasa mimi nashangaa huyu mbaba analia nini sasa wakati naendelea na kazi yangu ya kuosha vyombo mara bibi akatokea akamkumbatia huku akitaja jina lake mwanangu umekuja nae akaanza kulia. Ndo nikagundua kuwa kumbe huyu ndo baba yangu.

Bibi akanigeukia Lisa mwamkie baba yako aisee nilisikia kitu kama kinanikaba nikatengeneza chuki kubwa kati yangu na baba yangu najiuliza siku zote hizi alikuwa wapi. Nikamjibu bibi nimeshamwamkia ilikuwa mchaba kama saa sita hivi. Basi bibi na baba wakaingia ndani na mizigo ikaingizwa ndani mimi hata sikuwashobokea nikaendelea na kazi zangu bibi akaniita nami niingie ndani nikamgomea. Nilikasirika sana. Muda wa chakula ukafika bibi akaanda chakula huku anaimba nyimbo kuonyesha alivyofurahi kumwona mwanae. Wakapakua chakula nikagoma kula na baba nikamwambia bibi siwezi kukaa sehemu moja na huyu mbaba wao wanalia mimi nina hasira tu.

Babu wakati huo hakuwepo alikuwa amesafiri kikazi ameenda mjini make alikuwa na wadhifa kidogo serikalini. Jioni babu anarudi make babu alikuwa ananidekeza sana nilivyomuuona tu nikamkibilia na kumkumbatia namwambia kuwa kuna mbaba yupo ndani yupo na bibi wanajiliza wanadai ni baba yangu. Babu nakumbuka alinituliza na vijizawadi vya mjini. Ndo nikakubali kuingia ndani.

Baba alikaa kijijini kama wiki mbili hivi na alikuja na zawadi kibao kwa ajili yangu. Na kila akitaka kwenda sehemu ananibembeleza tunaenda wote. Hali hiyo ilipelekea kuanza kidogo kidogo kumzoea na kuamini kuwa ni baba yangu. Wakati wa kurudi kwenye kutafuta nakumbuka nilimsindikiza na mpaka mjini nililia sana kuona anaondoka na kuniacha alimbembeleza sana akiahidi kurudi kunichukua. Nikamkubalia akaondoka huku mapenzi ya mtoto yakazaliwa mpaka leo nampenda sana baba yangu hunambii kitu kwake.

Maisha yakaendelea kama kawaida kwa babu, tulikuwa tunaishi Maisha mazuri tu ya kawaida ila sio magumu sababu babu yangu kidogo alikuwa anajiweza yaani kwa ufupi pale kijijini tulikuwa wakishua.

Upande wa mama kwao napo sio mbali na pale kijijini kwetu nikijiji cha Jirani tu hivyo nilikuwa nikienda mara kwa mara kuwasalimia babu na bibi pia japo pia mama yangu nilikuwa simfahamu.

Nilikuwa darasa la sita sasa ukatokea msiba upande wa mama, mama mkubwa dada yake na mama alifariki alikuwa akiishi Dar es Salaam lakini nilikuwa namfahamu make akija Kijiji ilikuwa lazima aje nyumbani kwa babu mzaa mama kunisalimia na kuniletea zawadi za hapa na pale. Huyu nilikuwa namchukulia kama mama yangu. Mama alikuwa anaweza kuja kwao kutoka Dar na asije kwetu kuniona nitasikia tu mama yako alikuja na kuondoka hivyo moyoni mwangu hata hakuwepo. Ndugu upande wa mama niliwaona ni bibi, babu, mamamkubwa (aliyekufa) na mjomba make hao ndo walikuwa wakinijali na kuja kuniona mara kwa mara hivyo upendo wa mama sijawahi kuupata mpaka leo.

Endelea kuwa na mimi nitarudi.

 
Ya kweli ya kutunga!Kama ya kweli tiririka mfululizo.
ni kweli nitatiririka ila uwe mpole sababu nje ya jamii forum tuna majukumu yakutafuta riziki hivyo naoma uwe mvumilivu nitajitahidi kuandika visa virefuvirefu na kufupisha ili watu tujifunze kuna atakaejifunza kupitia mimi na mimi naweza jifunza kupitia comment zenu. asante
 
Aisee!
 
Pole sana aiseh!
Bora angalau ulilelewa na Babu na Bibi wa kweli yaani wazazzi wa baba yako!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…