Ep 11
Siku ya field imefika nimejiandaa nimeenda kazini kwa kina kaka Dev naanza kazi. Natambulishwa kama mdogo wake kaka Dav yaani nipo na furaha, Napata marafiki wapya. Maisha yanaendelea walau kipindi hichi nina nafuu nikiamua kupika napika, nikiamua kuacha hakuna wa kuniuliza nafanya chochote ninachojisikia kufanya najiona kabisa kaka Dav na untie wameniamisha kabisa sayari.
Pale kazini ninaendelea vizuri nimempata rafiki mpya mcheshi tumuite Husna. Muda wa lunch huwa tunaenda kununua na kuja kula pale kazini. Kuna sehemu ofisi imetenga kama sehemu ya kulia chakula. Hivi imekuwa ni kawaida yetu kwenda kununua na kuja kula pale kazini. Tofauti na kina kaka Dav wao huenda kula huko huko na kurudi.
Kaka Dav ananitambulisha kwa baadhi ya ndugu zao na mama yake kama mdogo wa ihari na mimi aunt anamfahamu kaka Dav kama kaka yangu wa ihari. Maisha ni mazuri siku moja kaka Dav ananitambulisha kwa girlfriend wake ni mzuri kwelikweli yaani Maisha yangu yamejaa amani.
Nimeshazoeleka pale kazini kuna kaka mmoja anaitwa Rafael. Rafael anajenga mazoea kidogo kidogo kwangu mara wakienda kula ataniuliza Lisa unakunywa soda gani namtajia wakirudi amenibebea.
Mazoea yakaanza kidogo kidogo siku nyingine ananibebea chips anamuita Husna ananiletea mimi na shoga yangu tunakula tu ikafika hatua ikawa kama sheria kila wakienda kula lazima arudi na chakula kwa ajili yangu.
Ikumbukwe Kaka Dav ameshanipa onyo kuhusu wanaume wa kazini pale. Ila mtu akikuletea kitu huwezi kukataa, pia kaka Dav ameshanionya pia kuhusu Rafael. Siku moja kama ilivyo kawaida ya Rafael kuniletea chakula siku hiyo kanibebea chips na soda, nipo na Husna tunataka kula. Mara kaka Dav anaingia huku amefura kwa hasira anakuja moja kwa moja kwangu hivi Lisa unataka nikuonye mara ngapi kuhusu huyo Rafael? Chips zile zote zimemwangwa chini ananifuata amenishika tai anataka kunipiga. Nimeogopa nimefumba tu macho nasubiri kibao kama si ngumi kitue kwenye mwili wangu. Nasikia ameniachia nafumbua macho nakuta ameweka mikono yake mifukoni huku amanikazia macho na kunambia nisamehe Lisa sikukusudia kukufanyia hivi ila sitaki uwe na mazoea na wanaume wa hapa watakuchezea tu mdogo wangu.
Hakuna shida kaka nimekuelewa naondoka zangu na kurudi ofisini kwetu. Nachukua simu na kumtumia ujumbe Rafael. “Samahani Rafael naomba usinunulie kitu chochote tena”
Unamwogopa huyo kaka yako?
Hapana namheshimu sitaki kumkwaza. Kidogo kidogo nikaacha mazoe kabisa kwa Rafael.
Maisha yanaendelea siku zangu za kukaa pale zimeisha inabidi nirudi zangu kumalizia masomo yangu. Kwakweli kilikuwa kipindi ambacho kilikuwa na nafuu Kwangu. Narudi kuendelea na masomo yangu.
Muda umefika nimemaliza chuo, nipo tu nyumbani kwa baba mdogo naona kidogo wamepunguza masimango nafanya kazi zote kama kawaida lakini ile kupigwa bila sababu hakuna tena kusimangwa hakuna. Kazi ikawa kupata kazi sasa. Kila siku wakina babamdogo na mke wake wananipa ahadi zisizotimia za kutafutiwa kazi lakini hamna mabadiliko.
Siku moja baba anakuja hoja niendelee na masomo tena Magogoni ninakubali lakini kwa sharti nikae hostel baba yangu ankubali anatuma pesa kwa mdogo wake. Nimeshafanya maombi ya hostel msimbazi centre nimepata nafasi na magogoni nimepata nafasi.
Ninapewa hela kwenda benk kulipa ada ya chuo, hela ya miwani macho yalikuwa yananisumbua kidogo na hela ya kununua vitambaa ya kushona suti kwa ajili ya sare. nimepewa sh 1.2 kwa ajili ya matumizi yote.
Ada za wadogo wangu huwa napewa mimi kwenda benk lakini siku hiyo nakutana na msiba mpya katika Maisha yangu. Nimeenda moja kwa moja posta bank ya CRDB tawi la Holland ilikuwa tarehe 17/6/2014 siku ya jumanne sijawahi kuisahau hii siku katika Maisha yangu
Lengo langu ilikuwa nilipie ada ya chuo laki sita, na ada ya hosteli laki tatu, nikitoka hapo ndio niendelee na mizunguko mingine. Nimeingia ndani ya benki nimechukua fomu ili nijaze tena mbele ya tela kabisa. Nipo bize naendelea na shughuli zangu akaja mbaba anaonekana mtu wa heshima amevaa suti na tai juu akanianamia na kuninong’oneza unalipa ada? Nikamjibu ndio sasa mwanangu naomba unisaidie na mimi nimekuja kulipa ada ya wadogo zako lakini sijui hata hizi fomu zinajazwaje nikamjibu sawa lete tu fomu nikujazie
Akaleta fomu ananitajia majina najaza kiasi nimjazia nikachukua slip zake nimempa naendelea na za kwangu nimemaliza niachukue pochi yangu hamna baasha nayo haipo nataamaki kumbe nimeibiwa napiga kelele mlango wa benki unafungwa watu walokuwa ndani ya benki hawaruhusiwi kutoka nje. Tumeenda kwenye CCTV Camera kuangalia kuanzia kipande cha mimi naingia ndani ya benki. Watu wote wanaonekana sura nikiwemo mimi ila yule baba aoniibia haonekani sura kuanzia alivyoingia mpaka anaondoka.
Kumbe wakati ananiongelesha alichukua mfuko kutoka kwenye mfuko wa suruali lake akaukunjua na kuchukua pochi yangu ilokuwa juu mahali naandikia na kuitumbukiza kwenye mfuko wake kisha anatoka zake nje yuule.
Nilipiga kelele kama kichaa nikaombwa namba ya baba akapigiwa simu aliongea tu kiustaarabu rudi tu nyumbani mwanangu kuibiwa ni kawaida mwenyewe nimeshawahi kuibiwa pole usiwe na wasiwasi.
Wakati naendelea kulia ndani ya benk kuna baba mtu mzima anaamua kunisaidia kuanzia kwenda kuangalia kwenye CCTV. Ananipeleka polisi central kutoa taarifa tunapigwa danadana. Tunaambiwa turudi kesho yake. Nawaza narudije nyumbani, baba nimeshaongea nae je wale watu yaani baba yangu mdogo na mke wake itakuwaje.
Baba ananipigia ananisisitiza nirudi nyumbani tena kwa upole. (NAMPENDA SANA BABA YANGU YEYE NI SHUJAA WANGU) basi narudi nyumbani ile kuingia ndani tu babamdogo anaanza ee Lisa kama ulikuwa hutaki shule si ungesema yaani hela hile yote umeenda kuionga si bora ungeiacha kaka yangu angefanyia kitu kingine. Simjibu nanyamaza tu. Baba kila muda ananipigia simu na kunambia usiwaze mwanangu haikuwa riziki ananitmia jumbe za kunitia moyo. Yaani baba hakunilaumu wala sijui kufanyaje kuhusu pesa ile mpaka leo kuna amani kati yangu na baba yangu. Namuomba Mungu aendelee kumlinda baba yangu.
Kila siku naenda polisi central hamna jipya zaidi ya kuambiwa kuwa upelelezi unaendelea. Na kila nikienda nampa baba yangu tarifa nachoambiwa baba akaniambia niache kwenda polisi hamna msaada wowote na nisahau kuhusu hiyo hela Maisha mengine inabidi yaendelee. Ila kuhusu shule itabidi nisubiri tena labda mwaka mwingine tena ajipange upya make sasa hivi hela imemuishia make analipa na ada ya wadogo zangu pia. Nimemwelewa baba na kuendelea kutulia nyumbani.
mchana mwema