MENEMENE TEKERI NA PERESI
JF-Expert Member
- Mar 11, 2022
- 5,392
- 14,646
Mwambie Kaka bila kusahau mwambie namiliki Corolla yenye number plate ya jina la ukoo Kaka.Mwamba MENEMENE TEKERI NA PERESI huyo hapo usichezee hiyo fursa huyo ni doctor , usije kusema hauna bahati tena.
Muhimu aheshimu unywaji wa ulazi tu , mbona fresh tu.. 😁😁😁😁Mwambie Kaka bila kusahau mwambie namiliki Corolla yenye number plate ya jina la ukoo Kaka.
Kumbe wewe ni mwanaume?Imebd nisitshe zoez la posa kuna jamaa huko juu anataka kutoa machozi.
😀Imebd nisitshe zoez la posa kuna jamaa huko juu anataka kutoa machozi.
Kikubwa ataje yeye mwenyewe mahali Kaka ,maana Mimi Sina harusi kubwa ni pale kwa mkuu wa wilaya tunamaliza kila kitu hakuna habari ya sijui ya brother sheikh Wala mchungaji ni mwendo wa kutia sahihi tu .Mkuu unijulishe robo ya gharama za harusi niachie ila pombe zisipungue 😁
hawa nao wahuni hachelewi kukupiga nusu kaputi huyu.Mwamba MENEMENE TEKERI NA PERESI huyo hapo usichezee hiyo fursa huyo ni doctor , usije kusema hauna bahati tena.
Dadakidoti ukiniangusha huu ulabu nitakuona wa ovyo mno.Kikubwa ataje yeye mwenyewe mahali Kaka ,maana Mimi Sina harusi kubwa ni pale kwa mkuu wa wilaya tunamaliza kila kitu hakuna habari ya sijui ya brother sheikh Wala mchungaji ni mwendo wa kutia sahihi tu .
Baada ya hapo ni gharama ndogo tu pale mapacha ya kunywa na kula Mimi na nyinyi Wana alafu usiku nikacheze sebene na Dadakidoti Ila nadhani ukiniwezesha hata laki mbili itakuwa pia Sana
Hiyo ni Sheria Ila nimekuwa najaribu kufanya utafiti kuhusu ulanzi na kukosa nguvu kwa joint za miguu aisee nimehitimisha kuwa sitakiwi kuendelea kunywa ulanzi nisijeshindwa kusimamia kucha kunako sita kwa sitaMuhimu aheshimu unywaji wa ulazi tu , mbona fresh tu.. 😁😁😁😁
Nipo hapa nasimamia hili amini kwambahawa nao wahuni hachelewi kukupiga nusu kaputi huyu.
haya buanaNipo hapa nasimamia hili amini kwamba
Pastor kaishia wapi??asante kipenzi niko imara sana. kipindi cha nyuma kitu kidogo tu natoa machozi kama nimefiwa ila sasa nipo tofauti kabisa sitoi machozi yangu ovyo tena. nikikutana na changamoto natulia kwanza ndio naitafutia ufumbuzi sio wa kulia lia tena.
sio pastor naomba nieleweke. nimesema mtumishi wa Mungu. kuna aina nyingi ya watumishi. labda ni mwimbaji, au mwinjilist au shemasi au vinginevyo. Achana nae huyo. sio kwamba nimeandika kila kitu mpenzi. nimeelezea tu kwa ufupi.Pastor kaishia wapi??
Mlokole wa watu
Ndio mkuu…Aint Woman.Kumbe wewe ni mwanaume?
Tunakupenda pia my dearEp 21
Siku zilienda Dav hakuamini kama ningesema basi. Nilirudisha pete kwa mhuisika Dav hakuamini kama ningemwacha nilimwambia kuwa siku ukiona umebadilika na unaweza kuniheshimu japo kidogo na kutulia utanitafuta ila sio kwa sasa Dav nahitaji kupumzisha akili yangu sasa. Nikikaa sawa nitakwambia ila sidhani kama naweza kukusamehe. Hivi hatujaoana Dav huko hivi ukiniweka ndani ukajua tayari nipo chini ya himaya yako itakuwaje. Kinachoniuma mwanamke yuleyule toka umepanga mpaka umejenga kwako bado tunakosana kwa sababu yake. Kitanda kilekile ninachokilalaiaga mimi bora mgeenda sehemu nyingine si hapa. Au ningewakuta sehemu nyingine sio hapa kwako ningekusamehe kabisa. Au angekuwa mwanamke mwingine siku ile si ulikana ukasema ulikuwa unampa hela ili akupikie na hapa alikuja kukupikia tena sababu unampa hela? Dav alilia sana, alinipigia magoti lakini sikujali kilio chake wala magoti yake niliondoka zangu nikawaacha kwenye kikao na nikaazimia kumuondoa Dav kabisa Dav kweye Maisha yangu na nilifanikiwa kumuondoa mazima.
Mahusiano yangu na Dav yalidumu kwa miaka mitatu na miezi minne na kipindi chote hicho japo ilikuwa long distance relationship sikuwahi kumsaliti wala kuwaza kufanya hivyo mpaka tunaachana. Nikawa bize na Maisha yangu japo ilikuwa ngumu lakini mwisho wa siku niliamua kukubali matokeo.
Maisha yana pilika pilika nyingi sana. Kwenye heka heka za hapa na pale nikakutana na kijana mwingine mtanashati ni daktari katika hospitali kubwa hapa dar alinisumbua kwa kipindi cha mwaka na zaidi. Nilishamtoa Dav kwenye akili yangu nikaamua kuwa naye ila kumbe yule jamaa alikuwa ameoa na ana Watoto watatu familia yake inaishi mkoani lindi.
Nilivyogundua tu sikutaka kuangalia nyuma wala sina cha kupoteza kwake nikakimbia futi mia. Hakuna mtu namwogopa kama mume wa mtu. Maisha yalisonga nilikaa single miaka miwili yaani mtu akiniambia habari za mapenzi simwelewi kabisa hata kidogo. Nikaamua kujikita kwenye kazi zangu.
Nikaja nikakutana na huyu mpendwa namaanisha mlokele ni mtu maarufu kidogo nikaanza nae mahusiano nikiamini huyu ni mtumishi wa Mungu hawezi kunitenda. Msinilaaumu jamani Lisa nakula nashiba kuna siku tulijikuta tumevunja amri ya sita hata sielewi ilikuwaje. Mungu naye hakuwa mbali jamani mimba hiyo. Nikalea mimba yangu mpendwa yule naye kumbe ni silent killer ana matukio yake pia. nikaamua sasa kuwa bize na mimba yangu.
Namshukuru sana Mungu alinijalia handsome boy mwanangu ana miaka miwili sasa ananipa kila sababu ya kupambana. Sasa hivi nina amani na katoto kangu nikiwa single mother.
Kuhusu nyumba ya antie aliyokuwa anajenga niliimalizia na document zake ninazo mimi siku yoyote akitokea nipo tayari kumpa pasipo kudai chochote kile.
Dav alikuja kuoa mwanamke mwingine lakini walishindwana. Walikatana mpaka mapanga wakapelekana mpaka mahakamani. Dav siku hizi ni chapombe ana midevu kama osama yaani usmat ule hana tena nilikutana mwaka juzi nilivyooenda kumsalimia baba tulikutana mjini bahati mbaya nikiwa na kichanga aliumia sana. Kuna siku huwa anamfuata baba yangu na kuanza kumsumbua baba kuwa mimi nimke wake anamtaka mke wake nilimwambia baba ampeleke polisi. Ila baba hataki anampenda Dav ila mimi nilishakula viapo na viapo siwezi kurudi tena kwa Dav. Simchukii nilishamsamehe kabisa ila pia simpendi namchukulia kama mtu wa kawaida tu.
Mama naye yupo south Africa kuna kipindi aliumwa sana alipata ajali akateguka mguu akawa anahitaji msaada wetu ndugu zake wakatwambia kuwa twende kumuuguza tukagoma sio mimi sio Joy alikubali kwenda south Africa kumuuguza ilibidi aende mdogo wake. Alivyopona tu alikuja Tanzania akatuomba msamaha, tulimsamehe hivyo alirudi south kuendelea na Maisha yake ila tuko poa kabisa. Joy naye anaendelea vizuri mwezi wa 7 tunatarijia kula ubwabwa mdogo wangu antarajia kufunga ndoa. Hatuna ukaribu wa kivile ila tunawasiliana japo kidogo kidogo.
Baba naye ndoa yake inapumulia gas walitengana chumba na mama yetu wa kambo na mdogo wetu ni mdangaji maarufu Morogoro mjini. Yaani ni ameshindikana. Kwa baba mimi na Joy tuliacha kwenda kabisa nina miaka mitatu toka nilivyoenda mwaka 2021 sijawahi kukanyaga tena. Nikimmisi baba yangu huwa najitahidi kwenda na mabus ya kufika mapema moro na mtoto wangu tunafikia ofisini kwa baba jioni tunaru zetu Dar naondoka juu kwa juu.
Katika hekaheka zote hizo nimefanikiwa kujenga kakibanda kangu kadogo kazuri japo si kivile lakini kanaridhisha kapo Mbezi Msumi. Nitaarajia kuhamia kabla ya pasaka mwaka huu. Nina amani furaha na afya njema mimi na mtoto wangu tuko poa kabisa.
Sijutii kuwa single mother sababu mtoto wangu ananipa kila namna ya kupambana na ndiye mtu pekee niliye naye katika Maisha yangu japokuwa ni mdogo lakini ananipa furaha. Nina amani na sasa hivi naufanyia kazi msemo wa Joy naishi ulimwengu wangu kabisa. Mwanangu ndiye dunia yangu.
Asanteni kwa kuwa na mimi, niliyemkosea au kumkwaza kwa namna moja ama nyingine naomba anisamehe. Na samahani kwa kuwachosha ila nina Imani kuna mtu japo mmoja amejifunza kitu kutokana na historia ya Maisha yangu.
NAWAPENDA!
Mwishooooo.
Tafadhali Mara nyingine ili neno my dear katika komenti ya uzi huu hususani kumuhusu huyu binti naomba usilitumie ndugu yangu .Tunakupenda pia my dear
Hilo jina nikajua ni bidadaNdio mkuu…Aint Woman.
Hili jna ni msemo wa kiarabu.Hilo jina nikajua ni bidada
Nakutaka radhi tafadhali ndugu yangu sikujua kama una maslahi hapoTafadhali Mara nyingine ili neno my dear katika komenti ya uzi huu hususani kumuhusu huyu binti naomba usilitumie ndugu yangu .
Maana linaweza kudhoofisha uhusiano mwema Kati yangu na wewe
Baba mchunga katika ubora wako🤣🤣🤣🤣Dadakidoti ukiniangusha huu ulabu nitakuona wa ovyo mno.