Kuna wengine hatujui tulipokosea

Umeshawahi kuuliza kwa ndugu na jamaa kwann hana mapenzi nanyi au hata yeye mwenyewe
Au kuna jambo kubwa mshua alilifanya dhidi yake kupelekea yeye mama kujenga chuki kwenu??
 
Pole Sana
Najua inauma kiasi gani
Nimeshindwa kwenda kijijini baada ya kumzika babu yangu mpendwa (alikuwa kama baba mzazi) na mama yangu mzazi. Sina appetite tena na huko 🥲
 
Pole Sana
Najua inauma kiasi gani
Nimeshindwa kwenda kijijini baada ya kumzika babu yangu mpendwa (alikuwa kama baba mzazi) na mama yangu mzazi. Sina appetite tena na huko 🥲
Kweli ,hata Mimi baada ya kuwazika wazazi wangu wote Sina mzuka na kijijiji,na likitokea Jambo sitaki kukaa muda huko,naenda chap na kurudi.
Nyie ambao bado wazazi / walezi wapi jitahidini kwenda kuwasalimia kila ikiwezekana.
Kuna siku zitafika unatamani kwenda Ila hawapo,inauma kichizi
 
Mm naona dada kuna mambo unatakiwa uyaache ili uishi na binadamu hapa duniani, deal na mambo yako tu, unapoanza kufuatilia simu za watu, na vitu vingine ndo hapo unapoharibu mambo, utajikuta unaishi kwa stress siku zote na binadamu wote utawaona hawafai isipokuwa wewe!
 
Umeshawahi kuuliza kwa ndugu na jamaa kwann hana mapenzi nanyi au hata yeye mwenyewe
Au kuna jambo kubwa mshua alilifanya dhidi yake kupelekea yeye mama kujenga chuki kwenu??
ndugu mpaka marehemu bibi (mama yake) walijitahidi kumweleza na kumwambia kuwa badae sisi ndio msaada kwake lkn wapi. na ana upendo sana kwa watoto wa ndugu zake. kipindi bibi yupo tukienda labda tukakutana na watoto wa mama zetu wadogo au wajomba zetu. utasikia wanamtaja utasikia auntie fulan tena wanamtaja kwa mazuri. aliwasomesha watoto watatu wa kaka yake mmoja na wote wana maisha mazuri lakini wamemdampo hawana msaada wowote kwake. wamewajengea wazazi wao mjengo wa maana yeye kaachwa kwenye mataa. lakini anavuna alichopanda
 
Kuna siku zitafika unatamani kwenda Ila hawapo,inauma kichizi
Sikuwah kuwaza hili katika maisha yangu. Ni kama meza imepinduka.
Mahali ambapo ilikuwa haipiti miez 3 nishaenda siku hizi hata hapanistui wala kupawaza.
Hata mzuka wa kulala pale ndani nimekosa kama ni msiba nazika nasepa na gar ya msiba
 
Hapa duniani huji kutana na binadamu asiye na mapungufu, japo mapungufu yanatofautiana!! Simu imesajiliwa kwa jina la mtu, ww unahangaika na simu ya mtu mwingine ili iweje? au mtu ahangaike na simu yako ili iweje?

Unamvizia mwanaume ili iweje? au yeye akuvizie ili iweje?

Wanaofanya mahusiano ya aina hiyo ni wale ambao bado wana utoto utoto, mtu mzima anaejielewa hawezi kuwa na mahusiano ya aina hiyo!!

Muda wa Dav kuoa ulikuwa haujafika ndo maana mama yake ndo alikuwa anafosi aoe, na ndo maana Dav alikuwa anaendelea na wanawake wengine kwakuwa muda wake kuoa ulikuwa bado.

Muda wa yeye kuoa kama umefika lazima atakuwa sasa ametulia na hana mambo mengi!!
 
huo ni mtazamo wako. Dav alioa tena ndoa ya kanisani. lakini haikudumu hata miaka miwili walipelekana mpaka mahakamani ndio walipopeana talaka. aliyekuwa mke wa Dav alinitafuta kabla ya kudai talaka nadhani alipewa stori kuhusu mimi na Dav na kesi zake zilikuwa kama zile ambazo nilishindwa mimi kuzivumiia. na aliyekuwa mke wake mpaka leo mpaka kesho tunawasiliana. namchukulia kama rafiki tu wakawaida. na yeye amepitia mengi labda kupita yangu. Dav harekebishiki.
 
ujue kuwa single kuna raha yake eti eti huna stress
Zawadi pekee ya mtoto wako kama wewe unaona kabisa sina utajiri mkubwa kama wengine wakubwa basi ni kumpa malezi Bora ya baba na mama.
Kuna raha ya mtoto wako kuona anapendwa Toka akiwa mdogo
 
Ila kama hujaolewa na Dav anataka kukuoa mkubali tu. atakuwa keshajifunza mengi. Na wewe pia una mtoto hivyo kama akitaka kukuoa mkubalie tu, chansi ya wewe kuolewa ukiwa na mtoto ni ndogo.

Ujana una mengi na wanaume wengi huwa wanafeli na wanapoteza wife material sababu ya ujana.

Binafsi namependa Dav we msamehe tu ila mpe masharti akiyafuata mkubalie tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…