Kuna wengine hatujui tulipokosea

Epi 4

Namweleza Hawa hisia zangu juu ya Omary pia namwambia alichoniambia dada juu ya kuwa na mahusiano kazini.

Hawa ujue Omary amenitongoza na mimi nahisi kumpenda sijui unanishauri nini. Sikia shoga yangu Lisa alichokwambia dada yako ni kweli hapa hawaruhusu mahusiano kazini. Pili Omary ni muongo hakupendi angekuwa anakupenda asingenitongoza mimi. Ujue na mimi amenitongoza. Lisa mimi simpendi Omary ila kama wewe unampenda sawa ila tufanye kitu kimoja usimkubali kwanza. Mimi nitamkubalia halafu nimwambie tutoke out na nikiwa nae nitakupigia simu uje ufanye kama unatufumania na hapo tutamuuliza kuwa kati yako na mimi anampenda nani. Naweza kumkatalia shoga.

Omary anafuata jibu lake namtolea nje wakati mwanzo nilikuwa nimeshaonyesha dalili za kumkubali. Namkatalia machoni lakini moyoni nampenda. Kila weekend nasubiri simu ya Hawa ili tumfumanie omary lakini sioni. Siku zimekatika kazi zinaendelea kama kawaida. Naanza kusikia fununu kuwa Hawa anatoka na Omary. Mapenzi ni kikohozi mwisho wa mtu nathibibitisha mwenye kuwa kweli wapo katika mahusiano. Nawaona wanakumbatiana nabaki tu kuumia sina cha kufanya. Nimemkataa mwenyewe nitamkasirikiaje sasa. Hawa nae sina cha kumfanya zaidi ya kukatisha ushoga.

Mapenzi yao yakokomaa mara Hawa ni mjamzito. Wakafunga ndoa ya bomani ni kwa kipindi kifupi tu. Lisa nikawa mpole nikawatolea wanaume wote walokuwa wananiwinda kwa sababu nilikuwa nampenda omary. (tutakuja kuwaona tena Hawa na omary mbele)fuatilia

Baba aibuka tena.

Mimi tayari namiliki simu kipindi hicho nokia toch baba ananipigia na kuanza kunigombeza Lisa aliyekwambia ufanye kazi kwa umri huo nani? Mbona hukunishirikisha? Namuomba baba anisamehe. Lakini yeye wala hakufikiria kwenye kusoma kwangu walioangaika ni babu na bibi tena yeye yuko bize. Na Maisha yake.

Baba anatoa amri kazi niache mara moja kwani natakiwa kurudi shule. Nampenda baba yangu kuliko kitu chochote atasema nini mimi nikapinga. Ndani ya wiki akatuma nauli ya mimi kutoka kanda ya ziwa na kwenda Morogoro kwa ajili ya shule.

Tukutane kesho Mungu akipenda muda wa kuwa na mtoto wangu sasa. Alamsiki.
 
ishaanza kukolea...inabidi ianzishwe forum mahsusi kwa hadithi(Simulizi mchanganyiko)
...
hizi za based on true story zina arosto moja kali hapa nasubiri nijue G, Rachel na mwamba patrickk wanafikia wapi
wakati huo mtoto wa Rachel akikua na mtoto wa G akue wajue mama zao ni mtu na dada kisanga
...
haya Dadakidot shusha vitu
 
Ep 5

Nakata tiketi ya kwenda Morogoro, naaga pale kazini kwa mbwembwe kuwa naenda kusoma. Utawala wananisihi sana nisiondoke kwani nipo kwenye orodha ya wafanyakazi wanaokaribia kupata ajira ya kudumu. Dada amenisihi sana lakini nimewagomea naikukumbuka sana nafasi hii.. Inabidi nirudi Kijiji kuaga na kujiandaa kwa ajili ya safari.

Nimefika kijijini babu na bibi wanalipokea vyema jambo la mimi kurudi shule lakini upande wa bibi mzaa mama inakuwa tofauti inakuja barua kwa babu ya kuzuia mimi nisiende Morogoro. Barua inaeleza Kwa sababu zifuatazo:-

  • Kuwa baba hana kazi maalumu ya kumuingizia kipato ni misheni town tu.
  • Baba hana mke hivyo mimi kama mtoto wa kike nani atakayeniangalia?
  • Baba hana nyumba ya kuishi.
Na nyingine kibao ila hizi zilikuwa zimetiliwa mkazo. Barua hii iliandikwa na mjomba kutoka upande wa mama naikukumbuka sana barua hii. Hapa ndo unapojidhiirisha msemo wa mdharau mwiba mguu huota tende.

Napokea simu kutoka kwa mama ni miaka sita imepita tangu tulivyoonana kwenye msiba hatujawahi kuonana tena ananipigia simu na kunambia nisiende Morogoro kwa baba atatuma nauli nimpe muda tu ili niende Dar. Nae namkatalia babu nae anajaribu kunishawishi lakini wapi.

Natishia kujiua kuwa hakuna wa kunizuia kwenda kwa baba yangu labda kifo tu. (wazazi wawekeni wazi Watoto wenu.) nampigia baba simu na kumwambia kuwa wanajaribu kunizuia nisije huko wanadai kuwa huna nyumba, huna mke, huna kazi utanitunzaje? Baba ananijibu kama nimekuzaa mwanangu nitashindwaje kukutunza. Alokwambia sina nyumba nani achana nao mwanangu wewe siku ya safari ikifika panda bus njoo mimi ni baba yako.

Naongea na babu ananiruhusu ila ananiambia nikikuta Maisha ni magumu nimpigie simu anitumie nauli nirudi kanda ya ziwa. Tunakubaliana siku ya safari inafika napanda bus kuja zangu Morogoro huku nikifurahi kuja kuishi na baba yangu na kuwaona wadogo zangu ambao nawasikika kwa majina tu.

Nipo kwenye bus Kidoti mie naenda Morogoro. Tumefika Dodoma kwenye siti ya pembeni abilia mwenzangu ameshuka na anapanda kijana mdogo tu age mate wangu anatoka zake Dodoma anakuja Dar ndo makazi yake. Tunasalimiana anajitambulisha kuwa anaitwa Dev si jina lake. Kijana huyu anakula hovyo. Ananunua vitu anakula kama mwendawazimu yaani kama kero tunakaribia Gairo Dev anaumwa tumbo nampa pain killer nilikuwa nazo. Dev anakaa sawa tunaanza stori za hapa na pale tunabadilishana namba wote tunashuka Morogoro tulifika usiku. Ananisubiri mpaka wenyeji wanapokuja kunihchukua naye aendelee na safari zake. Kumbe yeye anaishi Morogoro wote tunaenda Morogoro mjini tofauti mitaa tu japo si Jirani.

Ajabu anaekuja kunipokea msamvu sio baba yangu mzazi ni baba yangu mkubwa kaka yake na baba. Ananiambia kuwa baba yangu kasafiri kikazi yupo tanga akirudi atanikuta kwake. Nakubali nitafanyaje sasa na wakati mji huo sio mwenyeji na baba yangu.

ya kulalia tukutane kesho. nawapenda
 
Dah! Omary anaenda kula tunda kimasihara! 🤨🤨
 
Mimi ndio Omary, umenikera sana kutomalizia..
 
Ungebaki kazini jamani🥲
 
Dah, wa kishua halafu kwenda shule unakutana na mbwa mwitu 10?
Nwei tuendelee kustorika
Wakishua wa kijijini unawaju??

Kama ushawah kuishi kijijini ni rahisi kumuelewa mleta uzi.
Ushua wa kijini huwa ni tofauti ndogo tu kati ya makapuku na huyo wa kishua, huenda tu home kwao ndo kuna solar, au umeme au nyumba nzuri au mzee ana kakipato ka laki 3 kwa mwezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…