bila shaka mmeamka salama. lisa nimeamka sasa uchovu wa safari umepungua fuatana na mimi
Ep 6
Tumefika sehemu kwenye nyumba Fulani hivi dirishani nasikia bamkubwa anaita Beti! Beti… (si jina halisi) fungua uje umchukue mdogo wako akapumzike alafu utakuja nae asubuhi nyumbani. Huyu Beti ni dada yangu mtoto wa babamkubwa pale amepanga huwa anaenda kushinda kwao usiku anaenda kwake kulala.
Dada akanichukua akanipa maji nikaoga na kulala. Kumepambazuka asubuhi tumeamka tumeoga tunaenda kwa bamkubwa. Tumefika natambulishwa kwa wenyeji wangu yaani Watoto wengine wa bamkubwa na mke wake. Mke wake toka nipo mdogo huwa nasikia habari zake kuwa ni mjeuri sana na mkorofi. Baba yangu mkubwa ana Watoto wanne na kuna ndugu wa mamkubwa Watoto watatu jumla saba namimi nimekuwa wa nane. Yaani sio Watoto wadogo mabinti na vijana tupo pale.
Imeandaliwa chai tumekunywa pale. Mgeni nimepewa soda stori za hapa na pale na wenyeji wangu. Mazingira ya pale ni uswahilini sana babamkubwa ana nyumba mbili kubwa na ndogo za kawaida sana. Kubwa ina vyumba vingi kuna wapangaji wengi. Pia nyumba ndogo ni inaonekana ya zamani. Nyumba zote mbili hazina umeme wala solar. Kwenye nyumba kubwa kuna sebule ambayo wanatumia familia ya bamkubwa. Ila vyumba vyote vilivyobaki vina wapangaji.
Muda wa chakula cha mchana umefika. Umesongwa bonge la ugali hapo kwa bakubwa ni familia kubwa na mboga inawekwa kwenye bakuli moja imewekwa katikati juu ya ugali watu wanaizunguka sahani na kuanza kula. Lisa mbona sijazoea mambo haya jamani kwa dada nilipotoka ilikuwa self service na kwa babu japo ni kijijini hatujawahi kushare mboga bakuli moja. Hata hamu ya kula sina majamaa wanakula kama wapo vitani mpaka mama mkubwa alinionea huruma na kusema nitakuwa nakula nae. yeye ana chakula chake special hali na watoto wala chakula kama chao ndo ikawa pona yangu. nawaza baba arudi tu anipele kwake.
Naongea na baba kwenye simu ananiahidi ndani ya siku chache ataakuwa amerudi na atnipeleka kwake hivo niwe mvumilivu kidogo. Namimi nanvyompenda baba yangu nitaachaje kuvumilia sasa.
Muda umeenda jioni imeingia naona mamkubwa anawambia ndugu zangu wakawatandikie kuku. Nashangaa mapya haya sasa kuku wanatandikiwa vipi? Ngoja nione naona wanazunguka nyuma ya nyumba wanachukua viroba vimechakaa vimejaa kinyesi cha kuku. Kumbe vilikuwa vimeanikwa vinapelekwa ndani kwenye nyumba ndogo vinatandazwa chini kama kapeti na giza linavyozidi kuingia kuku wanarudi mmoja moja wanaingia ndani. Wana kuku kibao si chini ya kuku 50.
Usiku umeingia tupo nyumba kubwa sebuleni tumekula. Dada beti anapewa maagizo akamtandikie mgeni. Dada anaingia nyumba ndogo kule kulipotandikiwa kuku ana andaa mazingira baadae ananifuata lisa twende ukapumzike mdogo wangu. Nanyanyuka namfuata dada tunaingia ndani nyumba ndogo kuna kachumba kadogo kuna kitanda. Vyombo kibao mandoo kibao mkaa kila yaani makolokolo kibao naonyeshwa kitanda nikalale. Dada ameondo nimepanda kitandani kulala. Huku nimeanza kupakumbuka kanda ya ziwa. Kitanda kile kina wadudu kibao sijawahi kuwaona wala kuwasikia popote. Ukimuua ananuka. Nikipitiwa usingizi kidogo nageuka kitoweo wa wadudu hawa ambao sijui ni wadudu gani wamenikaribisha mjini Morogoro.
Kwa mara ya kwanza na mimi najua kuwa kweli usiku ni mzito hewa chafu ya kuku wadudu wananisurubu. Ukipitiwa na usingizi kuku akivurugwa unaweza msikia mara kakaupanda mguuni mara mkononi mpaka kichwani kuku hawa hawana adabu kabisa na wageni.
Naamka asubuhi vipele mwili wote umevimba nimeanza kuwa na vipele naamka, wenyeji nao wameamka wananiambia pole tunaona Ngozi yako haipatani kabisa na kunguni ona walivyokutoa vipele. Ndo nikagundua kumbe hawa ndo kunguni.
Siku zimesogea baba hatokei zaidi ya kunipiga kalenda ndo nagundua kuwa kumbe haya ndo yatakuwa makazi yangu hapa mjini Morogoro. Kuwa nitatafutiwa shule ila nitakuwa natokea pale kwenda shule. Nagundua pia kuwa kweli baba hana mke, wala nyumba anaishi Tanga kwa sasa na mke wake walishaachana na mke wake ameshaolewa na mwanaume mwingine na ana mtoto mdogo wa huyo mwanaume wake mpya. Baba amezaa nae mtoto mmoja tu.
Na stori fupi kuwa huyo mama yetu mdogo alieachana na baba ndo chanzo mgogoro kati ya baba na mama mpaka kufika hatua ya baba na mama kuachana. Mamadogo alikuwa akifanya kazi bar.baba akienda bar anaweza kulala huko huko. Mama aliposhindwa akamua kuondoka zake Dar kwa ndugu zake. Ila sasa hata huyo mwanamke ameshindwa kuishi na baba. Msjijali huyu mama angu wa kufikia tutakuja kumuona vizuri huko mbele.