Kuna wimbi la bidhaa feki nchini kuuzwa kwa bei sawa na bidhaa halisi; Mamlaka husika zinawalindaje walaji?

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
Je, umewai kuuziwa bidhaa feki au bandia kwa bei ya bidhaa halisi? Uchunguzi uliofanywa na 'wazalendo' umebaini kuongezeka kwa bidhaa feki sokoni ambazo zinauzwa kwa bei sawa na zile halisi jambo ambalo ni kilio kwa walaji.

Uchunguzi huo ambao unawasilishwa kwenye andiko hili kwa ufupi, ulijielekeza zaidi katika Mkoa wa Dar es salaam (70%) na maeneo mengine mbalimbali nchini asilimia (30%)

Kufuatia uchunguzi huo inabainika Mkoa wa Dar es salaam haswa kupitia soko la kibiashara Kariakoo ndio kimekuwa kitovu kikuu cha uingizaji na usambazaji wa bidhaa hizi bandia au feki hasa za kielektroniki, plastiki, vipodozi, vifaa vya ujenzi pamoja na mavazi.

Mfano wa bidhaa za kieletroniki ni pamoja na simu, vifaa vya simu, vifaa vya umeme kwa ajili ya matumizi ya ndani kama vile nyaya, soketi, extension, pia kwenye ujenzi baadhi ya bidhaa hizo ni kama nondo, misumari na vingine vingi, kwenye vipodozi na madawa maeneo ambayo ni changamoto nako kuna shida, hadi zipo dawa za meno feki, sabuni, losheni zinauzwa sokoni kwa bei ya bidhaa halisi.

Changamoto kubwa inayobainishwa na kubainika ni kwamba bidhaa hizi zinachangia kuharibu soko la bidhaa halisi na kuwaweka Wafanyabiashara waaminifu kwenye mazingira magumu hasa kwenye uwiano wa mapato huku walaji wengi wakibaki kuwa waathirika wa bidhaa duni wakidhani ni za kiwango cha juu.

Licha ya kuzoeleka kwamba bidhaa nyingi feki au bandia uuzwa kwa bei za chini ikilinganishwa na bidhaa halisi lakini uchunguzi unabaini uwepo wa walaji wengi ambao wamekuwa waathirika wa kuuziwa vitu feki kwa bei ya bidhaa halisi na wafanyabiashara wasio waaminifu.

Katika udadisi wa kizalendo inabainika bidhaa nyingi feki ambazo zinapatikana kwenye soko zimekuwa zikitoka nje ya Tanzania, huku pia bidhaa nyingine zikitengezewa na kuzalishwa ndani kwa kuwekewa rebo sawa na bidhaa halisi zilizopo sokoni au kuzalisha bidhaa zenye muonekano unaoshabiana.

Sababu zipi zinachangia changamoto hiyo?
Zipo sababu mbalimbali ambazo zimekuwa chanzo; ambapo sababu kuu zinazobainika kwenye uchunguzi ni uzembe au rushwa kwenye taasisi za udhibiti, maendeleo ya teknolojia ya ughushi, kukosekana kwa uwajibikaji wa kutosha katika kusimamia sheria. Ingawa sheria zipo, utekelezaji wake bado ni changamoto.

Tunatokaje kwenye wimbi hilo?
Kufuatia changamoto mbalimbali ambazo zimetajwa kama vyanzo, hakuna budi mamlaka na wadau mbalimbali kuchukua hatua zinazolenga kuleta muharobaini.

Msisitizo wa Mzalendo; Ni kuweka mifumo wa ufuatiliaji wa bidhaa (Traceability), kusisitiza utumiaji wa teknolojia kama 'QR codes' na nambari maalum za usajili hasa kwa wazalishaji wa ndani ili kurahisisha utambuzi wa bidhaa halali. Njia hiyo itasaidia Wananchi waweze kuhakiki bidhaa kwa kutumia simu ili kuepuka mtindo wa kuwahadaa kununua bidhaa feki kwa bei ya bidhaa halisi.

Pili, kuna umuhimu kwa mamlaka zilizopewa dhamana kuongeza uwajibikaji zaidi ili kuwezesha ufanisi wa ukaguzi na ufuatiliaji wa bidhaa kabla ya kuingia sokoni na baada ya kuingizwa kuingizwa sokoni, Serikali iwekeze zaidi katika vifaa vya kisasa na teknolojia za kidigitali kwa taasisi kama TBS, TMDA na TRA ili kubaini bidhaa feki kwa haraka, hasa mipakani na bandarini.

Lakini kwa kuwa katika uchunguzi inabainika uwepo wa mazingira ya uzembe na Rushwa, hivyo ni vyema Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini ikalipa umakini zaidi eneo hilo kwa kufuatilia mienendo ya Watumishi hasa wanahusika kwenye operesheni za ukaguzi na ufuatiliaji wa bidhaa.
 
Shida yangu kubwa ipo kwenye nguoooooo za dukani, nunua suruali elfu 15 inachuja, elfu 25 inachuja,elfu 35 inachuja, nimewahi kununia cadet elfu 60, nikafua mara moja tu,ikabidi iwe ya kuendea shamba. T shirst ndio nimeacha kununua,bora nivae jezi kila siku. Nilishashauri sasa tutengenezewe nguo kama tishu, unavaa mara moja unatupa.
 
Je, umewai kuuziwa bidhaa feki au bandia kwa bei ya bidhaa halisi? Uchunguzi uliofanywa na 'wazalendo' umebaini kuongezeka kwa bidhaa feki sokoni ambazo zinauzwa kwa bei sawa na zile halisi jambo ambalo ni kilio kwa walaji.

Uchunguzi huo ambao unawasilishwa kwenye andiko hili kwa ufupi, ulijielekeza zaidi katika Mkoa wa Dar es salaam (70%) na maeneo mengine mbalimbali nchini asilimia (30%)

Mkoa wa Dar, inabainika katika udadisi kwamba Kariakoo ndio kimekuwa kitovu kikuu cha uingizaji na usambazaji wa bidhaa hizi bandia au feki hasa za kielektroniki, plastiki, vipodozi pamoja na mavazi.

Changamoto kubwa inayobainishwa na kubainika ni kwamba bidhaa hizi zinachangia kuharibu soko la bidhaa halisi na kuwaweka Wafanyabiashara waaminifu kwenye mazingira magumu hasa kwenye uwiano wa mapato huku walaji wengi wakibaki kuwa waathirika wa bidhaa duni wakidhani ni za kiwango cha juu.

Licha ya kuzoeleka kwamba bidhaa nyingi feki au bandia uuzwa kwa bei za chini ikilinganishwa na bidhaa halisi lakini uchunguzi unabaini uwepo wa walaji wengi ambao wamekuwa waathirika wa kuuziwa vitu feki kwa bei ya bidhaa halisi na wafanyabiashara wasio waaminifu.

Katika udadisi wa kizalendo inabainika bidhaa nyingi feki ambazo zinapatikana kwenye soko zimekuwa zikitoka nje ya Tanzania, huku pia bidhaa nyingine zikitengezewa na kuzalishwa ndani kwa kuwekewa rebo sawa na bidhaa halisi zilizopo sokoni au kuzalisha bidhaa zenye muonekano unaoshabiana.

Sababu zipi zinachangia changamoto hiyo?
Zipo sababu mbalimbali ambazo zimekuwa chanzo; ambapo sababu kuu zinazobainika kwenye uchunguzi ni uzembe au rushwa kwenye taasisi za udhibiti, maendeleo ya teknolojia ya ughushi, kukosekana kwa uwajibikaji wa kutosha katika kusimamia sheria. Ingawa sheria zipo, utekelezaji wake bado ni changamoto.

Tunatokaje kwenye wimbi hilo?
Kufuatia changamoto mbalimbali ambazo zimetajwa kama vyanzo, hakuna budi mamlaka na wadau mbalimbali kuchukua hatua zinazolenga kuleta muharobaini.

Msisitizo wa Mzalendo; Ni kuweka mifumo wa ufuatiliaji wa bidhaa (Traceability), kusisitiza utumiaji wa teknolojia kama 'QR codes' na nambari maalum za usajili hasa kwa wazalishaji wa ndani ili kurahisisha utambuzi wa bidhaa halali. Njia hiyo itasaidia Wananchi waweze kuhakiki bidhaa kwa kutumia simu ili kuepuka mtindo wa kuwahadaa kununua bidhaa feki kwa bei ya bidhaa halisi.

Pili, kuna umuhimu kwa mamlaka zilizopewa dhamana kuongeza uwajibikaji zaidi ili kuwezesha ufanisi wa ukaguzi na ufuatiliaji wa bidhaa kabla ya kuingia sokoni na baada ya kuingizwa kuingizwa sokoni, Serikali iwekeze zaidi katika vifaa vya kisasa na teknolojia za kidigitali kwa taasisi kama TBS, TMDA na TRA ili kubaini bidhaa feki kwa haraka, hasa mipakani na bandarini.

Lakini kwa kuwa katika uchunguzi inabainika uwepo wa mazingira ya uzembe na Rushwa, hivyo ni vyema Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini ikalipa umakini zaidi eneo hilo kwa kufuatilia mienendo ya Watumishi hasa wanahusika kwenye operesheni za ukaguzi na ufuatiliaji wa bidhaa.
Hiyo ni kweli sana mfano,mimi na familia yangu tumeshauriana kutonunua tena jug za kuchemshia maji za umeme.
 
TBS wamekaa ofisini wanasubiri mishahara na posho, Nahisi hadi rushwa wanapokea kuruhusu hizi feki
 
Kwenye upande wa electronics hasa tv za hisense watu wanapigwa vibaya mno!
 
Uchunguzi uliofanywa na 'wazalendo' umebaini kuongezeka kwa bidhaa feki sokoni
mkuu hujasema ni bidhaa zipi izo?
zilikuwa ngapi na sasa ni ngapi? umewezaje kuzijua kama ni feki?
au ni porojo za mkahawani izi?
 
Back
Top Bottom