Huku maeneo ya kibamba/luguruni/ubungo Daresalam,maji ni janga la kitaifa.
Dawasa kwa makusudi kabisa,,
wanafunga maji kwa wanainchi hata mwezi mzima maji hayatoki bombani,
Na kama watayafungulia basi ni usiku Sana,,Kati ya saa 01:00 am hadi saa 5 ;00am.
Ili watu wengine washindwe kuyapata.,
Tena watafungulia kwa masaa matatu au manne then wanafunga.
Kama ulikuwa umelala basi utaoga jeuri yako.
Wanafanya haya yote kwa baraka zote za uongozi mzima wa luguruni/kibamba Dawasa pamoja na engineers wao wa mradi..
Lengo ni kutengeneza shida ya maji kwa wanainchi,,
Ili wao waweze kufanya biashara yao ya kuuza maji ,,kwenye magari ya maji mitaani.
Dawasa wana mradi wao wa kuuza maji uliopo kibamba kwa Mangi..
Mradi huu unahusisha kuuzia maji magari yanaoyouza maji ktk maeneo yote ya kibamba.
Hivyo basi,,kipindi cha maji kutoka kwenye mabomba majumbani,
umekuwa ni mwiba mchungu kwa biashara hyo ya maji ktk magari na bomba la Dawasa.
Hakuna mwanainchi atashughulika na gari ya maji kama maji bombani yanatoka.
Sasa wameamua kurudi tena kwa style ya kufunga mabomba ya maji majumbani,
Ili wao waweze kuuza .
Na sidhani kama hata hizo pesa za mauzo hayo,, zidhani kama ni kweli zinaingia serikalini,
Kuna dalili zote za upigaji kwenye pesa hizo.
Maana sio kwa kuhujumu vile wanainchi kuwanyima maji,,
ili Dawasa na wenye magari wafanye biashara ya maji kwa uwingi.
Dawasa huuza maji kwenye magari kwa bei ya 2000 kwa 1 unit..
Na wenye magari hupita na kuuzia wanainchi mitaani kwa sh 15,000 kwa 1 unit..
Dawasa kwa siku wanaweza kuuza units zaidi ya 500..
Jamaa wanapiga pesa ndefu Sana.
Huu ni unyama usiokubalika hata kidogo.
wanatengeneza shida ya maji kusudi ili hizi gari zipate kusambaza maji kwa wanainchi?
Tena wanauza kwa kuringa,kwamba ukihitaji maji unalazimika kununuwa zaidi ya units 3 ambazo ni 45000.(madumu 3 kwa pamoja)
Hawauzi dumu moja moja,,
Huu ni zaidi ya ujambazi unaofanywa na Dawasa na watu wao wa magari ya maji.
Yaani mnatufungia mabomba ya maji ili muuze maji yenu bei juu mitaani?
Maana maji yakitoka majumbani biashara ya magari haipati soko..
Inawalazimu kuhujumu wanainchi kwa kuwafungia maji yasitoke kwa wakati..ili wao wauze.
Dawasa luguruni kibamba ni jipu linalosubiri kutumbuliwa muda wowote..
RIP Magufuli.
Nakumbuka alishawahi kulisemea hili la Dawasa kibamba ,,
Na kwa kipindi chake likaisha kabisa,,
Maji yalitoka masaa 24/7..
Mwezi mmoja baada ya kifo cha Magufuli,
Dawasa walianza figisu za kuweka ratiba ya maji kwa kila eneo la luguruni/ kibamba,,
Kwamba kila alhamisi na j nne wanafungulia maji,
Kuanzia 00:00 am hadi kesho 06:00 am..wanafunga.
Lakini ratiba hyo kwa Sasa haifuatwi na wanafunga maji mwezi mzima.
Ili wanainchi tuteseke na shida ya maji ili tununuwe maji ya magari wanayosambaza.
Ukiwauliza kwann wakati wa Magufuli maji yalitoka siku zote tena 24/7 bila kukatika,,
Majibu ya kueleweka hakuna.
RIP Magufuli,,
Upigaji umerudi kwa kasi ya makombora ya Vladimir Putin..
Serikali imeweka mabomba kwa gharama kubwa,,
Lakini wapo watu wachache waliopewa mamlaka ya kuhudumia wanainchi,,wakihujumu juhudi za serikali..
Naomba serikali ya mama yetu Samia,,
Itupie macho luguruni kibamba kwenye suala zima la maji na hujuma zake kwa wanainchi..
Wanainchi tunateseka na huduma za maji ,,na maji yapo kwenye visima,
Ila watesi wetu wanatutesa sababu ya ufisadi wao na tamaa ya kuendekeza njaa zao.
Sent from my M2101K7BG using
JamiiForums mobile app