Kuna wizi una faida kubwa sana. Ungana nami katika stori hii

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
4,580
Reaction score
7,943
Nikiwa primary darasa la nne moja ya somo nililokuwa naangukia pua ni hesabu na hapo ndipo nilipotolewa kwenye tatu bora niliyokuwa naishika la kwanza, la pili na la tatu.

Nikawa mpiga chabo maarufu wa hesabu darasani mpaka nikabatizwa jina na kuitwa bunduki macho.

Nilifadhaika sana, kwa kuwa mzazi wangu hakuwa mtu aliyesoma (aliishia la 4 la zamani) basi hakujua kuwa kusomesha kuna ambatana na kumtafutia mtoto vitabu bora. Hakutununulia vitabu vya binafsi sisi watoto wake.

Nilichoamua ni kuiba vitabu vya hesabu ofisini kuanzia cha la 5 - 7, jipime za watu, hesabu kwa vitendo. Na nilifanikiwa kuiba daftari la Dada mmoja alilompa rafiki yake baada ya kumaliza shule.

Dada alikuwa anaitwa FARIDA, alikuwa mtu wa kwanza kwa somo la hesabu kitaifa darasa la saba miaka hiyo.

Secondary alipangiwa Kilakala nako alipata kuwa wa kwanza kidato cha 2 kwa hesabu kwa upande wa wasichana kitaifa. Kwa sasa sina taarifa zake.

Dada alijua kuzipanga hesabu kwenye counter book lake. Nilijifunza hesabu Mimi mwenyewe kupitia ile counter yake mpaka niliianza kujua vizuri. Nilipofika la 6 niliweza kufanya hesabu karibu zote za shule ya msingi.

Darasa la 7 nikapata A bora ya hesabu wilayani kwetu.

Farida popote pale ulipo njoo uchukue laki moja yako hapa. Mimi hunifahamu ila Mimi nakujua vizuri. Rafiki yako(jina kapuni) nilimuibia Mimi lile daftari lako matata.

Nilichaguliwa shule nzuri ya boarding form one kwa njia uliyoifungua.

Note: Vijana msiibe, mtafungwa.
 
Niliwahi ibiwa kiroba changu nachotumia kubebea Daftari za shule.. kilikua na Daftari za masomo,vitabu vya sayansi,jipime,kiswahili, Magazeti na Majarida ya sani.
Nilikaa mwezi mzima siandiki, na home hawakujua maana wangejua the late mama angenitoa kichwa..
Nami niliiba hadi nikaeneza daftar
 
Hiyo tunaita kusogeza. Haujaiba ulisogeza. Ahahaha
 
Nasikia yupo dar kutafuta maisha.
Mimi niliachana naye la 5 alihama shule kuhamia mkoa mwingine(Songea) baada ya baba yake kupata uhamisho wa kikazi.
Mzazi wake alikuwa askari magereza

Songea ni Wilaya mkoa ni Ruvuma. Ila kama uyo mtu alikaa Kota za Magereza ya Songea (Mahabusu) kuna uwezekano nimekaa nae kota. Maana nimekaa sana pale. Saaaana. Sasa sijui tu miaka ipi alivohama ilo darasa la 5.
 
Dah! mkuu umenifanya nilikumbuke daftari langu matata sana enzi nipo primary 90s.
Daftari lilicontain summary za topic mhimu, kanuni, solved qns za necta papers n.k

Basi bhana jamaa mmoja aitwae Malimbe akawa analitamani sana na kuapa kuwa ipo siku angeniimbia, kweli baada ya wiki mbili daftari langu likapotea ktk mazingira tatanishi tena karibu na necta...!

Weee aliamsha mizimu ya kwetu, nilifula hasira nikaiba podo na upinde wa mzee breki kwa huyo nyang'au nikawakuta familia nzima wanaumme wapo kwenye "kikome" wanakula, nilivuta upinde na mshale wenye sumu kumlenga yule jamaa huku nikiunguruma kama simba tayari kwa kuruhusu mshale!
Kwakuwa Baba yake alikuwa muwindaji aliielewa hasira yangu na sikuwa nikitania hata kidogo. Ilibidi atembee kwa magoti kuelekea kwangu akinisihi nishushe siraha yangu chini... Sikushusha mpaka pale niliporushiwa daftari langu na fasta nikatoweka mahala pale.
 
Duuuuhhhh, wewe noma, ni Mnyantunzu au Mkurya wewe?
 
Songea ni Wilaya mkoa ni Ruvuma. Ila kama uyo mtu alikaa Kota za Magereza ya Songea (Mahabusu) kuna uwezekano nimekaa nae kota. Maana nimekaa sana pale. Saaaana. Sasa sijui tu miaka ipi alivohama ilo darasa la 5.
May be unamfahamu.
 
Bila shaka jamaa ulimuacha anakula kipondo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah ,umenikumbusha mbali sana ,jinsi nilivyoibiwa daftari langu .
 
Dah Mimi nilikuwa mpole sana shule hadi kufika darasa la 5 nikaanza kuchangamka na kujichanganya na wenzangu home kidogo mambo hayakuw fresh daftri likiisha inakuwa shida sana kupata jipya basi nikawa najiongeza madaftari yakikusanya natafuta jipya ambalo alimeandikwa kurasa mbili naiba naenda kujaladia linakuwa langu iloo toka apo sijawai nunua madaftari had namaliza la 7 ila nilikuja kupata msala wa kuiba vitabu ofisi ya walimu wakati sikuiba nikaamriwa nilipe nililipa alafu nikarudi kuviiba tena vyote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…