Bonde la Baraka
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 4,580
- 7,943
Nikiwa primary darasa la nne moja ya somo nililokuwa naangukia pua ni hesabu na hapo ndipo nilipotolewa kwenye tatu bora niliyokuwa naishika la kwanza, la pili na la tatu.
Nikawa mpiga chabo maarufu wa hesabu darasani mpaka nikabatizwa jina na kuitwa bunduki macho.
Nilifadhaika sana, kwa kuwa mzazi wangu hakuwa mtu aliyesoma (aliishia la 4 la zamani) basi hakujua kuwa kusomesha kuna ambatana na kumtafutia mtoto vitabu bora. Hakutununulia vitabu vya binafsi sisi watoto wake.
Nilichoamua ni kuiba vitabu vya hesabu ofisini kuanzia cha la 5 - 7, jipime za watu, hesabu kwa vitendo. Na nilifanikiwa kuiba daftari la Dada mmoja alilompa rafiki yake baada ya kumaliza shule.
Dada alikuwa anaitwa FARIDA, alikuwa mtu wa kwanza kwa somo la hesabu kitaifa darasa la saba miaka hiyo.
Secondary alipangiwa Kilakala nako alipata kuwa wa kwanza kidato cha 2 kwa hesabu kwa upande wa wasichana kitaifa. Kwa sasa sina taarifa zake.
Dada alijua kuzipanga hesabu kwenye counter book lake. Nilijifunza hesabu Mimi mwenyewe kupitia ile counter yake mpaka niliianza kujua vizuri. Nilipofika la 6 niliweza kufanya hesabu karibu zote za shule ya msingi.
Darasa la 7 nikapata A bora ya hesabu wilayani kwetu.
Farida popote pale ulipo njoo uchukue laki moja yako hapa. Mimi hunifahamu ila Mimi nakujua vizuri. Rafiki yako(jina kapuni) nilimuibia Mimi lile daftari lako matata.
Nilichaguliwa shule nzuri ya boarding form one kwa njia uliyoifungua.
Note: Vijana msiibe, mtafungwa.