Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Leo nimemkumbuka John Pombe Joseph Magufuli. Jamaa alijua kututenda kama watu na taifa. Huwa siachi kujiuliza ni vigezo gani alitumia kuwapa mamlaka watu wanafiki na wa hovyo waliokuwa wkimsifia na kumchekea wakati nyuma ya pazia walikuwa wakimchukia, kumponda na kutamani afe kama iivyotokea. Jikumbushe wakati wa COVID-19 alivyokataa barakoa na chanjo na wakati wa mazishi yake wale wale wanafiki walivyovaa mabarakoa na kutuhhimiza tuchanje. Ni unafiki na utapeli kiasi gani. Sielewi wanangu vigezo alivyotumia jamaa huyu kuwapa hata kuwaachia madaraka wabaya wake waliokuwa wakimchuuza bila ya yeye kujua. Ama kweli kuchamba kwingi? Kweli kabisa, sifa nyingi zaweza kuishia kuwa kashfa tupu.