passion_amo1
JF-Expert Member
- Dec 3, 2023
- 1,828
- 3,922
Wakuu Heshima mbele.
Tangu kutokee sekeseke la kukamatwa kwa wanaodaiwa ni “madada poa” nimeona kuna haja kubwa sana kuwe na chombo huru cha kuchunguza mienendo ya jeshi la Polisi na Polisi kwa ujumla.
Video inayoonyesha wanaodaiwa ni madada poa wakiwa wanalalamika unyanyasi waliopotia. Wamefika kituoni wakapelekwa garage nafikiri tuliowahi kulala polisi tunaelewa garage ni sehemu ya namna gani.
Wamefika huko wanaambiwa anzeni kuvua nguo zenu, tanueni mapaja na mambo mengine mengi ya kutweza na kudharirisha utu wa mwanamke ambao kimsingi ni dada na mama zetu.
wengine wanadai walikuwa wakiomba msaada wa taulo za kike lakini walikuwa wakijibiwa kwamba tafuta njia ya kujisitiri unayoyajua. Na mwingine alikuwa akiambiwa nikufungulie Mlango uje chooni ili tumalizane.
Kiukweli aliyetoa hii Amri anapaswa kuwajibishwa kwa udharirishaji alioufanya.Polisi hawa hawa ambao mishahara yao tunaifahamu na maisha yao mtaani tunayafahamu ndio wamekuwa wakifanya vitendo ambavyo si sahihi katika jamii.
Kwanini pasiundwe chombo huru cha kushugulikia tuhuma hizi zinazofanywa na Polisi? Hii inachafua jeshi zima la Polisi, Kwanini watuhumiwa wananyimwa dhamana wakati ni haki yao?
Sijui ndugu yangu Abdul S Naumanga mnasubiri nini kushugulika na kesi kama hizi?
Yaani binti anamuona mama mtu mzima Makamu ya mama yake anavuliwa nguo na kuambiwa atanue mapaja?! Kweli Polisi limefikia hatua hii?
TUENDELEE KUAMKA NA KUPINGA UONEVU UNAONDELEA KWA KUENDELEA KUDAI KATIBA MPYA ITAKAYOTULINDA WOTE.
=====
Pia soma: Vita ya DC Ubungo na Makahaba: Mgongano wa sheria, haki na maadili