Viongozi wa Yanga wana uswahili mno, kazi kusikiliza maneno ya mashabiki pamoja na tambo za Manara badala kufocus kwenye malengo yao. Maneno ya mashabiki yakamuondoa Zahera pasipo kujali matokeo ya uwanjani. Zahera alikusanya point Saba za ligi akiwa na point sawasawa na timu ya Simba huku upande wa Yanga kimataifa wakienda mbali zaidi ya Simba katika msimu huo.
Lakini kuongea ukweli kwa kocha ikawa ni sumu kwa viongozi, ukijumlisha na maneno ya washabiki + watani wake kuwa mpira wa ovyo ovyo butu butu magoli ya bahati nasibu, kocha hafai, washabiki wakamzomea kocha+kurusha chupa. Kikafuata kutimuliwa kwake.
Zahera anatimuliwa akiwa amemaliza msimu kwa kushika nafasi ya pili kwa kikosi cha Yanga cha kawaida tu
Anakuja Luc Eymael unaona kabisa timu inacheza Kama washabiki wa Yanga wanavyotaka (mpira wa burudani) na nafasi nyingi zikawa zinatengenezwa lakini umalizaji ikawa ni tatizo. Baadae mashabiki Kama kawaida yao wakawa kama makocha wao wakaanza ooho kocha hajui kupanga timu, wachezaji wazuri anaweka benchi, akazomewa kocha kwenye mechi. Kilichofuata kocha akapanic kwa kutoa kauli zilizojawa na hasira.
Na hizo kauli zilizojawa na hasira ziliongea uhalisia juu ya mashabiki na viongozi wa yanga. Kwavile watu hawataki kusikia ukweli basi wakaona wamtimue. Lucy Eymael nae anafukuzwa huku akiwa na rekodi ya kufanikiwa kushika nafasi ya pili kwenye ligi.
Huyu kocha mpya nae anafukuzwa kwasababu ya maneno ya mashabiki na haji manara kuwa Yanga inapata matokeo kwa mpira magimbi huku huku Simba ikicheza mpira biriani.
Huyu kocha naye anahukumiwa kutimuliwa huku akiwa hajapoteza mechi hata moja huku akicheza mechi tano tu ligi.
Kipigo cha goli nne dhidi ya Simba ni mechi iliyochezwa na mashabiki na viongozi zaidi, kuliko benchi la ufundi. Mashabiki wanaanza kuulizia uwepo wa Morrison, Tshishimbi, Niyonzima, Banka. Pasipo kujua utimamu wa wachezaji husika. Washabiki wameleta presha presha kwa viongozi na benchi la ufundi kuhusu uwepo wa hao wachezaji.
Hapo unategemea kocha atafanya nini zaidi ya kusikilizwa matakwa ya mashabiki?
pengine mashabiki wangetulia pasipo kuonesha hisia zao kwa wachezaji wao, kocha angezichanga karata zake na kupata sare, kushinda au kufungwa magoli machache. (Rejeo baada ya kutolewa Morrison, Tshishimbi na Niyonzima.)
Mwisho nasema hivi, Simba itaendelea kutawala soka la Tanzania kwa zaidi ya misimu mitano kwa huu uswahili wa Viongozi wakiongozwa na mashabiki wa Yanga. Badala ya kujenga timu, mnabomoa timu kila mara halafu tutakaa kulalamika TFF wakati mambo mengine yapo wazi tu. Badala ya kutengeneza timu mnabomoa timu kila mara, mnataka mafanikio ya kufumba na kufumbua