Kunani ITV kutumika kutangaza utapeli? Ilianza na Vanila Village Njombe, ikaja Kaylinda na sasa inatangaza Vanila village Zanzibar.

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Wale matapeli wa Vanila village Njombe sasa wamehamia Zanzibar. Na ITV iliyokuwa ikiwatangaza wakiwa Njombe (Vanila village Njombe) ndiyo Sasa inawatangaza wakiwa Zanzibar (Vanila village Zanzibar).

Hawa ITV ndiyo waliohusika kuwatangaza Kaylinda waliochezesha upatu kwenye mitandao na kisha kukimbia na fedha za watu.. why ITV?
 
Hiyo Ni Biashara acha makasiriko
 
Wa kulaumiwa ni vyombo vya usalama na wanaozisajili hizo kampuni. ITV wao sio kazi yao kuwachunguza wao ukiwapa vibali wanarusha kitu
 
Tatizo ni kwamba Hao unaowaita matapeli wana nyaraka Zote za kuonyesha kuwa wanafanya shughuli zao Kihalali.

nionavyo mimi ITV hawana makosa yoyote, Ikiwa wamejiridhisha kuwa kampuni hizo zipo kihalali.
 
Kilichoharalishwa na serikali, media zinaanzaje kukiharamisha??
Wanadocuments zote zinazowaruhusu kufanya hizo shughuli, kwanini ITV iwatie shaka?
 
Kilichoharalishwa na serikali, media zinaanzaje kukiharamisha??
Wanadocuments zote zinazowaruhusu kufanya hizo shughuli, kwanini ITV iwatie shaka?
Kwa upande wa Kaylinda serikali imesema ilisajiliwa ili kuuza vyombo vya kielektroniki. Sasa kama ITV ingelikuwa makini ingelibaini kuwa Kaylinda haipaswi kuchezesha upatu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…