Kunani Makongo Juu kutojengewa barabara miaka nenda rudi?

Kunani Makongo Juu kutojengewa barabara miaka nenda rudi?

mweongo

Member
Joined
Aug 23, 2010
Posts
62
Reaction score
228
Eneo la Makongo juu wilayani Kinondoni, limekuwa na shida ya barabara kwa miaka mingi sana. licha ya eneo hili kuwa maa muhimu na maarufu., na kukaliwa na watu mashuhuri, limekosa barabara kwa muda mrefu sana. Makongo juu inapakana na kambi za Jeshi za Lugalo, Makongo na changanyikeni, pia inapakana na vyuo vikuu vya Aridhi na UD (Mlimani), pamoja na mlimani City. lakini ukifika huko barabara ni mashimo na makorongo tu.

Mbunge wa Zamani Halima mdee alipigia kelele swala la Barabara Makongo Juu lakini wapi hadi kaondoka hakuna bara bara. Makonda aliwahi hadi kupeleka magreda na kuaminisha wana makongo kwamba barabara zinajengwa lakini wapi kwanishida iko wapi?

Makongo kumejaa watu mashuhuri, wakiwemo Maprofesa mawaziri wa sasa na wazamani, wanajeshi nk lakini wam wote hao wameshindwa kuitetea.

Barabara zimejengwa kila mahali Dar es Salaam, Kawe, Goba, Changanyikeni, Madale Mwenge, Sinza nk lakini makongo kakuna shida iko wapi?

Wana Makongo wangoje MB wao mpy Mch. Gwajima labda atawakomboa.
 
Ila kweli hadi yombo uswahilini barabara za lami kila mtaa ila makongo juu hawana barabara ya lami mpaka leo kuna sababu ya ziada
 
Back
Top Bottom