Kunaulazima Rais aanzie miaka 40? mbona hawa walifanya makubwa kwenye umri mdogo.

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
1.Alexander the Great. Huyu jamaa alitawala Macedonia kuanzia mwaka 336-323. Alianza kutawala akiwa na miaka 20 tu. Huyu ndiye aliangusha utawala wa Waajemi ambayo ilikuwa dola kubwa sana. Utawala wake ulianzia Macedonia, Afrika kaskazini hadi India. Mji wa Alexandria Misri unaitwa jina lake.

2.Yesu. Huyu mtu alianza kuhubiri akiwa na miaka 29 hadi 33. Amefanikiwa kuunda dini kubwa kabisa duniani.

3.Muhammad, alianza kuunda uislam akiwa na miaka 40, bado kijana.

4.Gaddafi alianza kutawala akiwa na miaka 27.

5.Thomas Sankara, moja ya viongozi wa Africa wenye maono makubwa na aliyeifanyia Burkina Faso makubwa kwa muda mfupi alianza kutawala na miaka 33.

6.Kublai Khan founder wa Mongol empire alianza kutawala na miaka 35. Empire yake ilikuwa kubwa nafikiri haijawahi tokea.

7.Spiderman mwenyewe anafanya mambo makubwa japo ni kijana mdogo sana🙂🙂🙂

Alexander the great aliwahi sema "fortunes favors the bold' inaonekana boldness hupungua umri unavyoenda hivyo kunafaida ya kuwa na viongozi vijana. Tungeanzia 21 kama wabunge.

Kuna sababu yoyote ya msingi ya Rais aanzie miaka 40?
 
nyongeza...

Mfalme Josia.
Mfalme wa Yuda (649-609)BC
alianza kutawala akiwa na miaka 8 na akatawala kwa miaka 30.
Ndiye mfalme aliyefanya mambo makubwa ambayo wazee wake walishindwa hasa kwenye mambo ya imani ya Mungu wa waebrania.

Salim Ahmed Salim
alikuwa balozi bora huko misri akiwa na miaka 22.

ngoja wajuzi watujuze
 
Mifumo ya maisha duniani imebadilika sana ukilinganisha na miaka hio ya nyuma. Mifano yako mingi ni ya millennium iliyopita
 
UGaddafi na Sankara ni mifano ya Juzi tu mkuu. Unafikiri nini kimebadilika sana hadi wazee pekee yao ndio wawe wanafaa kuwa marais?
 
1.Alexander the Great. Huyu jamaa alitawala Macedonia kuanzia mwaka 336-323. Alianza kutawala akiwa na miaka 20 tu. Huyu ndiye aliangusha utawala wa Waajemi ambayo ilikuwa dola kubwa sana. Utawala wake ulianzia Macedonia, Afrika kaskazini hadi India. Mji wa Alexandria Misri unaitwa jina lake.

2.Yesu. Huyu mtu alianza kuhubiri akiwa na miaka 29 hadi 33. Amefanikiwa kuunda dini kubwa kabisa duniani.

3.Muhammad, alianza kuunda uislam akiwa na miaka 40, bado kijana.

4.Gaddafi alianza kutawala akiwa na miaka 27.

5.Thomas Sankara, moja ya viongozi wa Africa wenye maono makubwa na aliyeifanyia Burkina Faso makubwa kwa muda mfupi alianza kutawala na miaka 33.

6.Kublai Khan founder wa Mongol empire alianza kutawala na miaka 35. Empire yake ilikuwa kubwa nafikiri haijawahi tokea.

7.Spiderman mwenyewe anafanya mambo makubwa japo ni kijana mdogo sana🙂🙂🙂

Alexander the great aliwahi sema "fortunes favors the bold' inaonekana boldness hupungua umri unavyoenda hivyo kunafaida ya kuwa na viongozi vijana. Tungeanzia 21 kama wabunge.

Kuna sababu yoyote ya msingi ya Rais aanzie miaka 40?
Mkuu muhammad (S .A.W) Hajaunda uislam mkuu rekebisha hapo uislam ulikuwep kabla ya muhammad mkuu
 
Kwa jamii na utamaduni wetu hapa Tanzania ni vigumu watu kumchukulia Rais mwenye umri mdogo serious. Kimsingi hakuna sababu Rais hawezi kuanzia labda 27 years old.

Macron wa Ufaransa ana miaka 38 na anafanya vizuri.
 
Kuna kukataa ukweli alafu kuna kuongea vitu usivyovijua wewe umesoma wapi kwenye kitabu gani wakakwambia muhammad(s..a.w) ndiyo mwanzilishi wa uislam jitafakari kabla ya kuropoka
Wewe umesoma wapi kuwa s.a.w sio muaanzilishi wa hiyo dini??

Hivi unajua maana ya dini??

Kama Mohammed sio mwanzilishi he nani alianzisha hiyo dini??

Iman kitu BAYA sana
 
Wewe mkuu unasikitisha sana,

Unapoongelea imani ya mtu lazima uwe na elimu nayo

mimi nimesoma kwenye quran muhammad ni mtume kama mitume mingine mkuu sio mwanzilishi bali ni muendelezaji wa dini kwa generations na yeye ndiyo alikua the last mkuu

Kwa akili yako unajua kila dini huwa inaanzishwa na watu sio hivyo mkuu dini nyingine imekamilika haina shida hata kidogo kuanzia kwenye quran na ndiyo maana wamagharibi wanajaribu kuungamiza uislam lakini wanashindwa unajua kwanini wanataka kuusambaratisha uislam??
 
Na ndio mana nimekwambia Iman ni kitu kbaya sana??

Umejuaje au unaushahidi UPI kuwa uislam hujaanzishwa na MTU??

Pia unahakika gani au nipe source ya uhakika Hapa kuwa wamagharibi wana mpango wa kuumaliza uisalam?? Nipe ushahidi nani kasema na wapi?? Na ni vipi wanajaribu kuangamiza??

HIVI NIKISEMA UISLAM UMEANZA NA HICHO KITABU KINAIYWA QURAN UTABISHA KWA POINT GANI??

UISLAM NI DINI WAFUASI WA KITABU KINAITWA Qur'an, WAFUASI WA MWALIMU WAO MTUME S.A.W, NI KAMA WAKRISTU WAFUASI WA BIBLIA NA MWALIMU WAO YESU..MBWBWE ZINGINE NI MAIGIZO HAO NDIO WAANZILISHI WA DINI ZENU
 
Duuh haya mkuu ain't here for league mkuu wala sikulazimishi kuamini kama uko really curious katafute data mwenyewe naona hapa tutabishana bila faida
Ukweli NDIO huo..sibishani ila we ndio unabishaa
 
Mkuu mie naona tatizo ni kuwa RAIs akiwa kijana na akimaliza muda wake akiwa bado kijana BASI KUNA possibility NYING ZA KUKATALIA MADARAKANI

MADARAKA MATAMU ASIKWAMBIE MTU
Lakini kuna wazee nao ving'an'ganizi sana halafu ubaya wa wazee huwa na mitoto mikubwa na huona kuwa wanawajibu wa kuwaandalia future hivyo hutaka kuirithisha hii mitoto. Museveni mzee na anataka kurithisha nchi mwanae. Nguema hivyohivyi. Mizee mingine inayon'gan'gania madaraka ni kama Nguesso, Biya, Bongo na Muhabe hadi katolewa. Wazee wengine huwa wa na bonge la extended family inayowategemea. hapo kunakuwa na nepotism ya kufa mtu.
 
Mkuu muhammad (S .A.W) Hajaunda uislam mkuu rekebisha hapo uislam ulikuwep kabla ya muhammad mkuu
Hapa mkuu tunazungumzia kutoka Secular point of view. Ukitililia maanani hilo Yesu na Muhammad wanakuwa ni watu wenye ushawishi walioweza kuanzisha dini kubwa.
 
UGaddafi na Sankara ni mifano ya Juzi tu mkuu. Unafikiri nini kimebadilika sana hadi wazee pekee yao ndio wawe wanafaa kuwa marais?
Wengi wakizeeka wanahofu ya maisha kwa hiyo njia yao pekee ya kuwa na furaha ni kusalia uongozini hata kama nguvu zimewaisha.Robo tatu ya viongozi waandamizi serikalini ni wazee overhead 60+ .......
Pia tabia ya wanaccm ya kuleana uzeeni na kuona vijana ni wanamapinduzi wataharibu nchi.
 
Lakini kuna wazee nao ving'an'ganizi sana halafu ubaya wa wazee huwa na mitoto mikubwa na huona kuwa wanawajibu wa kuwaandalia future hivyo hutaka kuirithisha hii mitoto. Museveni mzee na anataka kurithisha nchi mwanae. Nguema hivyohivyi. Mizee mingine inayon'gan'gania madaraka ni kama Nguesso, Biya, Bongo na Muhabe hadi katolewa. Wazee wengine huwa wa na bonge la extended family inayowategemea. hapo kunakuwa na nepotism ya kufa mtu.
Museven na Mugabe walianza kuongoza wakiwa na miaka mingapi??
 
Dr. Salim Ahmed Salim kaanzia huko Misri na 20 yrs..Ila Mimi napendekeza waongeze umri kufikia 60 years ile nafasi si ya mchezo mchezo..
 
Back
Top Bottom