1.Alexander the Great. Huyu jamaa alitawala Macedonia kuanzia mwaka 336-323. Alianza kutawala akiwa na miaka 20 tu. Huyu ndiye aliangusha utawala wa Waajemi ambayo ilikuwa dola kubwa sana. Utawala wake ulianzia Macedonia, Afrika kaskazini hadi India. Mji wa Alexandria Misri unaitwa jina lake.
2.Yesu. Huyu mtu alianza kuhubiri akiwa na miaka 29 hadi 33. Amefanikiwa kuunda dini kubwa kabisa duniani.
3.Muhammad, alianza kuunda uislam akiwa na miaka 40, bado kijana.
4.Gaddafi alianza kutawala akiwa na miaka 27.
5.Thomas Sankara, moja ya viongozi wa Africa wenye maono makubwa na aliyeifanyia Burkina Faso makubwa kwa muda mfupi alianza kutawala na miaka 33.
6.Kublai Khan founder wa Mongol empire alianza kutawala na miaka 35. Empire yake ilikuwa kubwa nafikiri haijawahi tokea.
7.Spiderman mwenyewe anafanya mambo makubwa japo ni kijana mdogo sana🙂🙂🙂
Alexander the great aliwahi sema "fortunes favors the bold' inaonekana boldness hupungua umri unavyoenda hivyo kunafaida ya kuwa na viongozi vijana. Tungeanzia 21 kama wabunge.
Kuna sababu yoyote ya msingi ya Rais aanzie miaka 40?