Kundi jingine la Houthi laishambulia Israel kutokea Yemen

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
1,831
Reaction score
5,489
Waasi wa kundi la Houthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen walitoa video ya kile walichokisema kuwa ni kurusha makombora ya balestiki katika Israel.

Msemaji wa jeshi la Houthi Brigedia Yahya Saree, alidai kurusha makombora ya balestiki na ndege zisizo na rubani dhidi ya Israel, akisema hiyo ni operesheni ya tatu ya aina hiyo na kwamba wanapanga kufanya mashambulizi zaidi "hadi uvamizi wa Israel huko Gaza utakapokoma".

Mapema mwezi huu, jeshi la wanamaji la Marekani lilinasa makombora matatu yakisafiri angani yaliyorushwa kuelekea Israel na kundi la Houthi.

Isreli inasubiri nini, kama inaweza kwenda lebanon kuwapa kifinyo hezbollah inashindwaje kwenda yemen kuwatia adabu wahuoth hao wanaojitia kiherehere kuingia vitani na israel?
 
Hilo haliwezi kuwa na madhara sana kwa sababu kijografia liko mbali sana na Israel.
 
Yemen ikaanza kupewa dozi km wale magaidi wa wapelestina Gaza.
Mtakuja kusema Israel inawaonea.
 
wavaa kobaz wanavituko sana wanaishiaga kusema tu Mungu mkubwa kama vile wengine hawana Mungu!
 
Waasi wa kundi la Houthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen walitoa video ya kile walichokisema kuwa ni kurusha makombora ya balestiki katika Israel.

Msemaji wa jeshi la Houthi Brigedia Yahya Saree, alidai kurusha makombora ya balestiki na ndege zisizo na rubani dhidi ya Israel, akisema hiyo ni operesheni ya tatu ya aina hiyo na kwamba wanapanga kufanya mashambulizi zaidi "hadi uvamizi wa Israel huko Gaza utakapokoma".

Mapema mwezi huu, jeshi la wanamaji la Marekani lilinasa makombora matatu yakisafiri angani yaliyorushwa kuelekea Israel na kundi la Houthi.

View attachment 2800907
Waandae vikombe vya uji kwani uji wao uko jikoni unachemka.

Tena yale mabalasi makubwa yale wanayotumia kutawadhia
 
Back
Top Bottom