Kundi la damu linaweza kubagua chakula? Mwanangu akila samaki anapata vipele na kujikuna. Nifanyeje?

Kundi la damu linaweza kubagua chakula? Mwanangu akila samaki anapata vipele na kujikuna. Nifanyeje?

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Mwanangu ana umri wa miaka miwili kasoro!

Ana uchu wa samaki kinoma!

Lakini bahati mbaya kila akila samaki anajikuna na kutokwa vipere mwili mzima mithili ya kupitiwa na mdudu washawasha!

Je, nitumie mbinu au dawa gani ili mwanangu aendelee kula samaki bila shida hii ya kujikuna (allergy /mzio)?

Msaada tafadhali wazazi wenzagu!
 
Duh! Pole sana kwako na kwa mwanao. Mimi nilikuwa nikimuosha tuu samaki hasa tasi na baadhi ya samaki wa maji chumvi nawashwa sana mpaka nachukua kitana kujikuna au brush, nikaambiwa nina allergy niache kutumia baadhi ya vyakula pomoja na chips mayai🤭😋 lakini ilikuja kuisha yenyewe hiyo hali. Sasa hivi kila halali nakula.
 
Ni samaki wa aina yote wanamdhuru? (Maji chumvi na ziwani?)

Kama wanaomdhuru ni wa maji chumvi basi uwe unampa sato/sangara na wengine wapatikanao ziwani and likewise.

Pole kwa baby
 
Pole sana kwa tatizo hilo. Je, ni samaki aina gani akila anajikuna? Nakushauri uende hospital kwa ajili ya kupima ni allergy zipi alizonazo mwanao.

Lakini pia, dawa ya allergy ni kuacha kukitumia kinachokuletea hiyo allergy. Yaani aache kuwatumia samaki.

Kama unaona kuna ulazima wa mwanao kupata virutubisho vinavyopatikana katika samaki (Omega 3) basi fanya mbadala wa kupata vyakula vyenye virutubisho sawa na samaki kama mbegu za Chia, almonds, karanga za Macadamia, nk
 
Duh! Pole sana kwako na kwa mwanao. Mimi nilikuwa nikimuosha tuu samaki hasa tasi na baadhi ya samaki wa maji chumvi nawashwa sana mpaka nachukua kitana kujikuna au brush,nikaambiwa nina allergy niache kutumia baadhi ya vyakula pomoja na chips mayai🤭😋 lakini ilikuja kuisha yenyewe hiyo hali. Sasa hivi kila halali nakula.
Hukutumia dawa yoyote hata tone
 
Pole sana kwa tatizo hilo. Je, ni samaki aina gani akila anajikuna? Nakushauri uende hospital kwa ajili ya kupima ni allergy zipi alizonazo mwanao...
Asante kwa ushauri
 
Mimi samaki yoyote nikimla lazima nitoke mapele mwili mzima. Hospitali nilijaribu kila dawa ikashindikana, so nimeamia tu kutokula. Nenda hospital wanaweza kukupa msaada na mara nyingi sisi wenye group o+ ndo tatizo tunakuwa nalo zaidi
 
Halafu kutapika kwenu ni kugusa tu mnarudisha Mwaaah
 
Mwanangu ana umri wa miaka miwili kasoro!

Ana uchu wa samaki kinoma!...
1 Ana kundi gani la damu.

2.Ni vema kuchunguza kwanza ni aina gani ya samaki akila ndo zinampa tabu? Je Ni samaki wa maji chumvi au
Ni samaki wa maji matamu
 
1.Punguza kiasi cha chumvi kwenye chakula cha mtoto

2. Usimlishe samaki wa maji chumvi
3. Usimlishe kitimoto
 
Duh! Pole sana kwako na kwa mwanao. Mimi nilikuwa nikimuosha tuu samaki hasa tasi na baadhi ya samaki wa maji chumvi nawashwa sana mpaka nachukua kitana kujikuna au brush,nikaambiwa nina allergy niache kutumia baadhi ya vyakula pomoja na chips mayai🤭😋 lakini ilikuja kuisha yenyewe hiyo hali. Sasa hivi kila halali nakula.
Alikuwa tasi nwenye vidoa vidoa?
 
Duh! Pole sana kwako na kwa mwanao. Mimi nilikuwa nikimuosha tuu samaki hasa tasi na baadhi ya samaki wa maji chumvi nawashwa sana mpaka nachukua kitana kujikuna au brush, nikaambiwa nina allergy niache kutumia baadhi ya vyakula pomoja na chips mayai🤭😋 lakini ilikuja kuisha yenyewe hiyo hali. Sasa hivi kila halali nakula.
Sijawahi kusikia mwanamke ana allergy na dudu la yuyu, Wala mwanaume ana allergy na Tukuyu
 
Mwanangu ana umri wa miaka miwili kasoro!

Ana uchu wa samaki kinoma!

Lakini bahati mbaya kila akila samaki anajikuna na kutokwa vipere mwili mzima mithili ya kupitiwa na mdudu washawasha!

Je, nitumie mbinu au dawa gani ili mwanangu aendelee kula samaki bila shida hii ya kujikuna (allergy /mzio)?

Msaada tafadhali wazazi wenzagu!
Ni baadhi tu ya samaki mkuu. Sio samaki wote. Mfano hao sangara wengi wana shida nae. Chunguza samaki mmoja mmoja. Achana na yule samaki mliezoea kumtumia hapo home.
 
Back
Top Bottom