Kundi la damu na kupata mimba

Kundi la damu na kupata mimba

Mkumbizi

Senior Member
Joined
Dec 31, 2013
Posts
171
Reaction score
26
Kuna uhusino wowote kwa makundi ya damu ya mwanamke na mwanaume kusababisha kushindwa kupata mimba kwa mwanamke endapo wataoana hasa kwa kundi (mwanaume) A negative na (mwanake)B negative kushindwa kupata mtoto.
 
sina uhakika kama kuna huo uhusiano ila nitarudi tena baadaye kwa maelezo mengine muda nawahi kwenye maombi...
 
Kuna uhusino wowote kwa makundi ya damu ya mwanamke na mwanaume kusababisha kushindwa kupata mimba kwa mwanamke endapo wataoana hasa kwa kundi (mwanaume) A negative na (mwanake)B negative kushindwa kupata mtoto.

damu group hazizuii kupata mimba ispokuwa utapata ila itaharibika mapema, mama akiwa Rh postive na baba akiwa Rh negative na Baba akawa Rh Positive bila kujali A au B au AB ni ni Majanga, hasa mama akipata mimba ya mtoto wa kwanza amnae Rh postive. mimba ztakazofuata ztaharibika zote otherwise achomwe sindano ya kinga iitwayo ANTI-D
 
Sawa kwahiyo nawashsauri watu kupima Rh kabla ya kuoana. Ni muhimu sana
 
Nimewapata vizuri nawahukuru kwa melezo yenu na ushauri mbariwe sana.
 
Mkuu BARIADI-KWETU naona umenichanganya kidogo. Matatizo mengi ya kundi la damu ni kwenye kundi la damu la Rh factor. Katika kundi hili unaweza kuwa Rh +ve au Rh-ve. Takwimu zinatuonyesha kuwa Rh-ve ni wachache kama asilimia 5 kwa population yetu hii ya Kitanzania. Mama akiwa Rh-ve na baba akiwa Rh+ve kuna uwezekano mkubwa kuwa kichanga kitakachobebwa na mama kitakuwa kundi la Rh+ve. Mara nyingi mtoto wa kwanza anaweza kukua bila matatizo na kuzaliwa akiwa na afya nzuri. Tatizo linatokea hivi, wakati wa kujifungua kuna uwezekano wa chembe chembe nyekundu kutokea kwenye kondo la nyuma (placenta) kuingia kwenye mfumo wa damu ya mama. Hapo mama ataweza kutengeneza antibodies ambazo zitaleta matatizo katika mimba zinazofuatia ile ya kwanza. Ndio maana ni muhimu kujua kundi la Rh la mja mzito na wale wenye Rh -ve wanadungwa sindano ya Anti D ili ku-mask chembe chembe nyekundu za Rh+ve zisije zikachangia kutengeneza antibodies. Sindano hiyo hudungwa ndani ya masaa 72 baada ya kujifungua.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom