Uchaguzi 2020 Kundi lipi litawaadhibu/ kuwabeba Magufuli na Lissu katika sanduku la kura?

Uchaguzi 2020 Kundi lipi litawaadhibu/ kuwabeba Magufuli na Lissu katika sanduku la kura?

Kwani We unaishi Ulaya au huu uchaguzi ni Wa Ulaya Ongelea Mazingira yanayokuzunguka yaani Mabeberu yameafanya hata kufikiria lazima uwaze Ulaya hahahhaa
Kwa siasa zinazofanyika nchini, hasa na chama chakavu, nakubaliana kabisa na yale maneno ya yule kocha wa YANGA, aliyowaambia mashabiki!! Ndio ukweli huo kwa sisi waafrika!! Yaani mtu anaibiwa fomu ya uteuzi, anaenda polisi, anapewa rb, kumbe fomu iliyoibiwa ipo polisi!! Anaambiwa mbona sahihi zinatofautiana? Upuuzi kama huu wapi dunia iliyoendelea utakutana nao? Waafrika uwezo wetu wa kufikiria una matatizo sana, ndio maana watu kama LISU, wanaonekana kama wakorofi kwani akili yake inaendana na za watu weupe!!! Hata wakenya kidogo wanaenda kwenye dunia iliyostarabika kidogo, ndio maana kiongozi kwao kusemwa vibaya sio inshu, lakini nchini ile bora umseme mungu vibaya kuliko kiongozi yule!!!
 
Wasalaam wana bodi,
Poleni sana na majukumu ya kulijenga Taifa.

Nchi yetu inaelekea katika uchaguzi mkuu na tayari mbiu imekwisha lia na amsha amsha za hapa na pale zimeanza.

Kuanzia tarehe 27 Agosti, 2020 hadi 28 Oktoba 2020 itakuwa kipindi cha mnyukano majukwaani kwa wagombea kutoka katika vyama vya siasa zaidi ya 10 katika nafasi ya Urais.

Katika kipindi hiki wanasiasa ambao wanaonyesha kuleta ushindani katika uchaguzi wa mwaka huu ni Mwanasheria nguli na mwanasiasa wa muda mrefu Ndugu Tundu Antipas Lissu kupitia CHADEMA na Rais anayemaliza kipindi cha utawala wake wa miaka mitano Ndugu. Dr. John Pombe Magufuli ambaye ameomba tena ridhaa kupitia chama chake cha CCM kuwa Rais kwa kipindi kingine.

Katika uchaguzi kura huwa katika makundi na wanasiasa makini katika kunyakua kura hizi za uchaguzi hurusha sera zao wakijikita katika makundi yafuatayo:

1. Vijana

2. Wakulima

3. Wafanyakazi

4. Wakina mama

5. Wafanyabiashara

Najua kampeni hazijaanza ila wagombea wengi walishaanza kutoa dodoso za nini watafanya. Wanasiasa walioingia ulingoni tumewajua.

Unadhani katika hao wawili niliowataja hapo juu ni mgombea yupi ambaye ana haiba ya kushawishi makundi hayo matano hasa ukizingatia mazingira ya KIUCHUMI(MICRO&MACRO), KISIASA na KIJAMII tuliyonayo kwa Sasa kuelekea uchaguzi?

#UCHAGUZI2020
#VISION2025
#AGENDA2063

View attachment 1549949View attachment 1549950
Sory mkuu kwenye picha huyo lisau ni yupi na huyo magufuli ndie yupi[emoji134]
 
Kwa Hali ya nchi yetu kundi ambalo magu atakuwa na uhakika ni wakulima na wakina mama na wakulima ndo wengi na akina mama ambao ni watu wagumu Sana kubadilika wakisema moja wanashikilia moja lkn kwa vijana, wafanya biashara na watumishi ni ngumu Sana watu wana maumivu na vilio sana Juu ya utawala huu
Wamachinga au?
 
Back
Top Bottom