GE2025 Kundo: Rais Samia ni kiongozi mwenye dhamira ya kweli, amebeba matamanio ya Watanzania, kwa miaka mitano ameongea kwa vitendo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Septemba 21, 2025 Mamia ya wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na makada wa chama hicho wakiongozwa na mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi mjini, Kundo Andrew Methew wamefanya maandamano ya amani kwa lengo la kuhamasisha wananchi kumchagua rais Samia Suluhu hassan kutokana na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati nchini

"Daktari Samia suluhu Hassan ukimuangalia machoni kwake unamuona ni Kiongozi ambaye anadhamira ya kweli ambaye amebeba matamanio ya watanzania ambaye kwa kipindi cha Miaka mitano ameongea kwa vitendo, Vitendo hivyo tumeviona kwenye barabara, tumeviona kwenye afya, tumeviona kwenye mawasiliano, tumeviona kwenye umeme"- Amesema Mgombea Ubunge CCM Jimbo la Bariadi Mjini Kundo Andrew Methew

Your browser is not able to display this video.




​
 
Ignored
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…