Kunenepa.

wa baha ela

Member
Joined
Jan 20, 2013
Posts
37
Reaction score
5
Sina mawazo na ningependa kuongezeka mwili kidogo, je? nitumie vyakula gani au nifanye kitu gani?..Help pliz, money isn't a problem.
 
Njia zinazo weza kukusaidia kuongeza unene





Sijui ni kwa nini unauliza dawa za kunenepa badala ya kuuliza njia zinazoweza kukufanya unenepe,kumbuka madawa yana side effects zake zinazoweza kuwa hatari pia kwa afya yako mfano kama unavyoona dawa za uzazi wa mpango.



Pia ni vema ukajua athari za unene kabla hujaanza kutumia siyo tu kwamba umbo lako litabadilika kabisa tofauti na ulivyo na unavyo tegemea mfano unataka unenepe kiasi ukajikuta umenenepeana nyama zinaning`inia tu lakini ujue unaanza kunyemelewa na magonjwa kama pressure nk.


Hata hivyo kuchagua kuwa mnene au mwembamba ni uamuzi wako binafsi,ila ningekushauri utumie njia za kawaida kuongeza unene kuliko madawa.Hata hivyo hatujui wembamba huo ni wa kuzaliwa nao,au unatokana na maradhi mwilini,au msongo wa mawazo.....ukishajua chanzo ni mwanzo wa kumaliza tatizo.


Njia zinazo weza kukusaidia kuongeza unene


1.Kula chakula cha kutosha kila unapokula halafu chenye mafuta mengi,chakula chenye wanga zaidi nk.
2.Usikae muda mrefu bila kula chakula,muda kabla ya mlo mwingine usizidi masaa 4 au 3 halafu ukipata msosi kandamiza sawasawa.
3.Achana na mazoezi hasa yale ya kukimbia.
4.Kula chakula kingi kabla ya kwenda kulala.
5.Punguza mawazo
6.Punguza kula mboga za majani na matunda badala yake kandamiza nyama,maharage nk.

Kutimia njia za kawaida ni bora kwa sababu ukiona uzito umezidi unaachana na njia

hizi lakini unene wa dawa wakati mwingine hata kama ukiacha kutumia zinakuwa

zimeathiri mfumo wa asili wa utendaji kazi wa mwili huenda ukashindwa kuzuia tena

Mkuu.@
wa baha ela Ukitaka kunenepa kula kila siku Ufuta mweupe ubwie mdomoni pasipo na

kupika kwa muda wa mwezi Mmoja utanenepa ile mbaya yake jaribu kisha uje hapa unipe

feedback.



 
Dr MziziMkavu, mafuta mengi na sedentary lifestyle ni risk factor ya magonjwa mengi kama vile ilivyo unene wa kupindukia. Nadhani kufanya mazoezi kutamuongezea hamu ya kula.
 
Last edited by a moderator:
hi, samahani mkuu nimeona hapa ulimshauri ndugu yetu ufuta mweupe ningependa kujua kwanini mweupe na kuna tofauti gani kati ya mweupe na ule wa rangi rangi?? thankx
 
hi, samahani mkuu nimeona hapa ulimshauri ndugu yetu ufuta mweupe ningependa kujua kwanini mweupe na kuna tofauti gani kati ya mweupe na ule wa rangi rangi?? thankx
Ufute mweupe ndio unao nenepesha kila kitu kina utaratibu wake masnai
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…