Kungekuwa na mpango ili tuweze kufuga swala, nyumbu etc

Kungekuwa na mpango ili tuweze kufuga swala, nyumbu etc

Unaweza kufuga. Ila unatakiwa kupata kibali kutoka MALIASILI. Kuna mwaka fulani, kule Sumbawanga kuna mtu alifuga. Ni jambo zuri sana katika kuhifadhi bionuai. Serikali yetu ingeweka sheria kuwa kila mwekezaji mwenye kiasi fulani cha eka za ardhi ya shamba; mfano kuanzia eka 500, basi lazima atenge eneo la hifadhi ya viumbe asili, ikiwa pamoja na wanyama pori. Nadhani, AFRIKA KUSINI wanafanfanya katika mashamba, sina uhakika kama ni sheria au matakwa ya mtu.
 
urasimu wa kupata vibali unatakiwa kupunguzwa. lengo la vibali liwe ni kuzuia ujangili na si kuchuma pesa. baadaye ufugaji wa hao wanyama uwe kama wa mbuzi na ng'ombe. pia vyuo vya kilimo na ufugaji vingepewa dili ya kuzalisha na kusambaza.
 
Pale, SUA, ukienda utapata maelezo yote. Fika kitengo cha kuendeleza mifugo kipo Kushoto kwenye kona unapoingia baada ya kulipita GETI LA SUA. ni kama mita mia na hamsini kivi kutoka hapo getini, Vinginevyo, ulizia hapo langoni. Upande wa kulia utaona kuna miche ya miembe, basi wewe ingia katika majengo yaliyo kushoto. Hapo ukiwamaambia unatafuta NDEZI wa kufuga, basi unaelekezwa kwa Profesa anayehusika na huo mradi. Atakupatia melezo kwa kina pamoja na manufaa KIBIASHARA.
 
wakuu nimemsikia leo Mh Rais akizungumzia hili suala. Ametuhimiza kufuga wanyama wa porini. Nasubiria utaratibu uwekwe na Kigwanala ili nianze kufuga Mbarapi.
 
Back
Top Bottom