- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Nimekuwa nikisia mara nyingi kuwa kunguru akifa haozi, bali hukauka tu na kadiri siku zinavyozidi kwenda hupukutika mpaka kuisha ila huwezi kuta kaoza wala kutoa harufu.
Badhi ya watu huwa wanasema haozi kwa sababu hali chumvi japo sina hakika katika hili maana mara kibao amekula vyakula vyenye chumvi kama nyama na vyakula vingine hapa home.
Je kuna ukweli wowote katika hili? Kama ni kweli sababu ni nini?
Badhi ya watu huwa wanasema haozi kwa sababu hali chumvi japo sina hakika katika hili maana mara kibao amekula vyakula vyenye chumvi kama nyama na vyakula vingine hapa home.
Je kuna ukweli wowote katika hili? Kama ni kweli sababu ni nini?
- Tunachokijua
- Kunguru ni ndege wakubwa kiasi wa familia Corvidae. Aina (Spishi) nyingine huitwa vinubi. Wanatokea mabara yote isipokuwa Antakitiki. Spishi nyingi ni nyeusi au mchanganyiko wa rangi kama nyeusi pamoja na rangi nyeupe, kijivu au kahawia; nyingine zina rangi mbalimbali kama buluu, pinki n.k. Hula karibu kila kitu kama vile ndege wadogo, wadudu, mizoga, matunda, nafaka n.k.
Kumekuwa na Hoja kuhusu kunguru zinazodai kuwa akifa haozi, hanuki wala kutoa wadudu huku ikidaiwa baada ya kufa hukauka tu na kupukutika mpaka kuisha kwa mzoga wake. Baadhi ya madai hayo tazama hapa, hapa, hapa na hapa
Je, ukweli wa hoja hizo ni upi?
JamiiCheck imefatilia maisha ya kunguru na kubaini kuwa Kunguru ni ndege kama walivyo ndege wengine ambao huishi na kufa kwa sababu mbalimbali ikiwemo magonjwa au uzee.
Katika kutafuta uhalisia wa hoja zinazodai Kunguru akifa haozi au kunuka JamiiCheck imemtafuta na kuzungumza na Afisa habari wa TAWA Beatus Maganja ambaye ameeleza kuwa hoja hizo hazina ukweli kwani hakuna kiumbe kisichooza baada ya kufa, akieleza hizo hoja ni imani tu ila hazina ukweli wowote.
"Hizo ni imani za watu tu huko mitaani na zipo nyingi sana! Kunguru ni kiumbe kama wengine, anaugua, anakufa na anaoza kama wengine. Hali yake kunguru mwenyewe na mazingira aliyopo ndio huamua muda gani utatumika tokea kufa mpaka kuoza kwake".-Afisa habari wa TAWA Beatus Maganja