Kwanza niseme! Kuna tetesi Hawa kunguru weusi waliletwa hapa inchini (MIJINI) kwa ajili ya kampeni ya usafi (Enzi za W/Mkuu Edo-lowassa)!
Kama ni kweli, Wataalam walioidhinisha lifanyike Hilo Basi walikurupuka!
Ebu waza kunguru mweusi anapora Hadi tonge la nyama mkononi, Ebu waza kunguru wanachukua nyama hata ikiwa jikoni wanafunua na kudokoa;
Yote tisa Hawa Kunguru weusi sasa wamegeuka kero kubwa Sana kwa sisi Wafugaji wa Kuku wa kienyeji!
MFANO Kuku Mtetea,Unamtunza vizuri anaatamia mayai 22 (Unatamani uyale mayai lakini unawaza soko la kuku), anatotoa vifaranga 18 , Hadi vifaranga hao wakue kunguru anakuwa kashapunguza vifaranga 17 kwa kuwala!
Mimi Kama mfugaji nabakiwa na kimoja tu, hapo sijazungumzia gharama ya chanjo ya Mdondo n.k!
Na ili Kuku awe wa kienyeji lazima akale chakula cha kuparua, ukimfungia kuku wa kienyeji hakui haraka na Ni rahisi Sana kufa kwa magonjwa!
Je; Nitumie mbinu/dawa gani ili vifaranga wasiliwe na Kunguru?
Toa maoni kwa faida yako pia maana msipotushauri namna ya kutokomeza Hawa Kunguru, Sisi Wafugaji tutapandisha bei, Msishangae siku KUKU wa kienyeji tukaja UZA LAKI MOJA!
Naombeni maoni yenu wadau, Vinginevyo mtaendelea kula mabloiler ya kuku wa Kizungu huko mtaani mpate kansa, Hususani kwa wapenda virigisi ambako sumu zote za kuku bloiler hukimbilia!
Tushauriane hapa kuondoa Kunguru mweusi ili bei ya KUKU wa kienyeji ishuke tukuuzie wewe mlaji hata kwa 5000/= ule firigisi,utumbo na kuvunja mifupa!
KARIBUNI KWA MAONI JAMANI