Kikwapa si ugonjwa mkuu! Inaitwa kikwapa kwa sababu ni harufu kali, tena isiyopendeza. Lakini kwa kweli ni harufu ya kuzaliwa nayo mtu, ni harufu ya mwili, au tuseme ya ngozi ya mtu. kila mtu ana harufu yake. Kuna watu wana harufu kali sana, na wengine wana harufu za wastani, nk. Sasa huyu mwenye harufu kali sana ndo huwa tunasema ana kikwapa. Yeye hata aoge namna gani harufu hiyo haitoki kwa sababu ni harufu ya mwili/ngozi/maumbile. Kumbe inabaki palepale tu. Ndo mana wanaojijua wana hiyo hali wanajitahidi kwa usafi na marashi ili kupunguza makali.
Kwa wale kina mimi wasiojijali au hawana uwezo basi harufu hiyo inakuwa kali kweli. Na mbaya zaidi mtu awe mchafu hajijali basi ndo hivo tena. Ananuka kwelikweli. Cha maana tuvumiliane kwamba tuko tofauti. Pili, tusaidiane kushauriana ili kuboreshana pale tunapokutana na wenye kikwapa. Mpe ushauri, mwambie afanyeje, atumie marashi gani, nk. Kwa hili wanawake ni mabingwa kuliko wanaume.