Kununua body za Hiace

Kununua body za Hiace

Mtoto Tajiri

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2014
Posts
300
Reaction score
173
Habari wana jamii!

Mimi nataka kujikita zaidi kwenye biashara ya Daladala lakini kwa mtazamo wangu nimepiga gharama za Hiace mpya ni 20m-25m, ni hii bei hadi kukulipa inachukuwa mda usiopungua mwaka au zaidi, lakini mimi nataka niwe nanunua mabodi ya hiace yenye kila kitu kasoro Engine tu may be kwa bei ya 5m then naweka Engine mpya 3L ama 5L. Total cost inakuwa 10m-12m.

Hapo vpi wana Jamii?
 
Hayo maswali mawili hapo juu tu ni changamoto tosha.
Gari kukuta frame yake inakila kitu ni tatizo,halafu pia tambua unaweza kuwa unakwepa kutoa Milioni 20 - 23 kununua mpya,ukajikutandani ya mwaka huo umetoa zaidi ya hiyo bila kujijua.Na mbaya zaidi hata ukienda Hopsitali utakuta Valve za moyo zimelegea kwa kuwaza kimeo cha kuungaunga.
Ingekuwa kama 10m mtu anasimamisha gari na kuwa na amani basi wengine wangemudu kununua hiaces.
Nakushauri,kama unataka ku cut off cost,nunua hiace yenye bodi nzuri hata kama engine imekufa au mbovu then nunua engine mpya na sio used kisha funga,hapo angalau utakuwa na amani.
 
Ok,
Body ukiipata kwa hiyo bei itakua imeshaisha kabisa!! Yaani kutu za kutosha tu na pengine inadaiwa vibali vya miaka chungu nzima TRA. Hivyo kuirudisha barabarani utahitaji hela za kutosha tu nazo!
 
Back
Top Bottom