I like this statement!
"If you dont try, it will forever remain impossible"
Kwa Mara ya Kwanza niliagiza SIMU (xiaomi mi 8 lite) china tena kwenye website amabayo sio maarufu,
Nakumbuka nilipitia online market nyingi Sana za china, nakazikuta za kitapeli na watu washapigwa Sana tu, Ila baada ya utafiti wangu na kujiridhiasha nikafanya malipo na Mzigo ukifika na nimesha fanya nao biashara zaidi ya maramoja
Ushauri juu ya thread yako.
Moja ya vigezo vya kampuni feki kwa uchunguzi wangu Ni:-
1. Bidhaa kuuzwa Bei mdogo Sana
Wakati natafuta simu nilikuta website moja hivi unauza simu, sumsung s 9+ $200. Na ukinunua Moja unapata nyingene buree! Weeeeee! Nilishtuka nikaanaza kuwa na wasi wasi wakati ukiangalia amzoni Ni $ 500 mpaka $600.
Vivyo hivyo kwa magari.
Mfano: gari la mwaka 2003 wanauza $450, wakati website zingine ambazo zinafahamika kwa uaminifua na wanauza gari hiyo hiyo yenye sifa Kama zile wanauza $ 1020. Kuwa makini tapeli hao,
2. Promotion kibao, pamoja na kuwa na Bei mdogo halafu Wana promotion kibao,
Bei wameandika $ 450, then wanakuambia watakupa spea tairi, tool box, and free shipping, hapo kuwa makini.
3. Mode of payment, Kuna mifumo ya ulipaji wa fedha ambayo ni ngumu kumtrak( kufuatilia) mfano; westunion, ukilipa umeliap no follow-up
Ila mfumo Kama PayPal, unaweza kumfatilia na pesa yako ikarudi,
Fanya tafiti, jiridhishe, fanya malipo naamini uatafanikiwa Ila ukiona dalili za utapeli, acha usilazimishe.
Thanx.