Kununua Gari la "Diplomat" - Zipi gharama nitakazopaswa kulipia?

Joined
Nov 17, 2011
Posts
40
Reaction score
7
Wasalaam,
Naomba msaada kwa anayefahamu.
Ninataka kununua gari kutoka kwa mfanyakazi wa Ubalozi hapa Tanzania. Gari limesajiliwa kwa namba za kibalozi T---CD---. naamini huwa magari haya yanakuwa hayajalipiwa baadhi ya kodi.

Gari lina taarifa hizi;
Aina - Land Cruiser Prado
Mwaka wa kusajiliwa - 2008
Mwaka wa kutengenezwa - 2008

Natanguliza shukurani
 
Yes Mkuu, kwa uelewa wangu mdogo kuhusu kodi unazotakiwa kulipia nafikiri ni IMPORT DUTY ambayo DIPLOMATS wanakuwa EXEMPTED. lakin kwa uhakika zaidi tembelea website ya TRA (Tanzania Revenue Authority - Home) or nenda ofisini kwao kujua zaid. Asante
 
Nafikiri hapo mkuu ni kufika TRA walifanyia tathimini hilo gari kwa hali ya sasa ili kupata thamani yake kisha kulipa kodi ambayo ilikuwa exempted.ukisha lipia ndipo utapata usajili kwa namba za kawaida pengine wachangiaji wengine wataleta michango zaidi
 
Kwa kawaida Diplomats huwa hawalipi Import duty, excise duty wala VAT, wewe ambaye sio diplomat ukinunua utatakiwa kulipa. Kwenye website ya TRA kuna price list yao (TRA) na calculator ya tax ikionyesha pia na depreciation, iangalie hiyo utapata overview ya kodi. Pia huwa inawezekana kunegotiate na TRA kuhusu kiasi cha kodi, ingawa mara nyingi huwa ni wagumu sana kuelewa. Ukienda vizuri unaweza kulipa kiasi kidogo zaidi cha kodi kuliko kile ambacho ungelipa ukiimport mwenyewe.
 
Ni kweli hiyo utalipia hizo cost zote,na CIF yake ni zaidi ya $25000 maana ni 2008 model..siyo pesa ndogo ulizia kwanza TRA maana utaratibu wao uwa haueleweki,ulizia CIF ya gari hilo ni kiasi gani maana ni sawa na kuli importu pya..ni sawa na zile gari unazozikuta showroom lakini hazijalipiwa tax
 
Hivi inakuwaje kuhusu kodi ukinunua gari la serikali ambalo limepata ajali au wame ya phase out?
 
Maelezo haya ni sahihi.

Kodi utakayokutana nayo unaweza ukajuta.
Sio mara zote. Gari la mwaka 2008 kwa sasa lina umri wa miaka mitano, haliwezi kuwa expensive kiasi cha kumtisha mnunuzi.
 
Magari ya Ubalozi/UN Agency mazuri ila Kodi yake Lazima ukae
Inategemea vigezo kadhaa
1. Imetumika muda gani
2. Inauzwa ikiwa katika hali gani
3. Kodi inakokotolewa kutokana na hayo hapo juu
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…