Kununua guta (Toyo au Wanhoo)

Kununua guta (Toyo au Wanhoo)

Spectophotometer

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2019
Posts
295
Reaction score
468
Wakuu habari ya leo.

Nina wazo la kununua guta la pikipiki kati ya Wanhoo au Toyo.

Nafikiria kumpa mkataba kijana kwa hesabu ya 20,000/= kwa siku kwa muda wa miezi 24. Eneo la kazi ni Tanga Mjini.

Wadau wenye idea na biashara hii naomba muongozo wenu.

Natanguliza shukrani.
 
Hio kitu inauzwa Sh. Ngapi na baada ya hio miezi 24 faida yako ni kiasi gani boss?
Nimeulizia dukani mpya kabisa ni kama 5.2mil(water cooling system) na body ni kubwa kidogo. Zile za zamani ni kama 4.8mil(Fan cooling system)
 
Wewe nunua chombo weka njiani, dereva akizingua wewe piga chini weka mwingine, Mungu akubariki mkuu.
 
Nipe kazi boss nimechoka kitaa kutwa kuchwa JF kuangalia utopolo wa Leecuu na mboeee
 
Biashara ya Vyombo vya moto inahitaji Dereva makini sana na mwaminifu.. Otherwise ukiendesha mwenyewe faida ni uhakika
 
Sema chochote mkuu, kwa faida ya wengi. Unauza guta hizo au una uzoefu nao members wakupigie kwa ushauri?
Hapa kuna matapeli wengi sana. Wanasubiri tu wakati muafaka. Mimi nashangaa sana watu wanaotaka kuanzisha biashara badala ya kufanya research huko site wanakuja kufungua thread hapa.

Siyo vibaya kuanzisha thread lakini unaanzisha ili kujazia mambo madogo madogo tu lakini siyo unaulizia uelekezwe kila kitu.
 
Hapa kuna matapeli wengi sana. Wanasubiri tu wakati muafaka. Mimi nashangaa sana watu wanaotaka kuanzisha biashara badala ya kufanya research huko site wanakuja kufungua thread hapa. Siyo vibaya kuanzisha thread lakini unaanzisha ili kujazia mambo madogo madogo tu lakini siyo unaulizia uelekezwe kila kitu.
Ni kweli mkuu. Lakini kama ulifuatilia uzi toka mwanzo utaona mtiririko wangu wa hesabu. Lengo langu tushauriane na tutatue changamoto kwa pamoja.
 
Back
Top Bottom