Kununua Nyumba Vs Kujenga Nyumba

Kununua Nyumba Vs Kujenga Nyumba

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Ndugu zangu;

Kwa desturi yetu sisi watanzania,kumiliki mjengo ni moja kati aya ndoto za watu wengi na pia ni kama kipimo cha kiwango cha ukwasi(Networth).Katika kutafuta maisha wengi wetu tunafikiri kwamba kupanga nyumba ni umaskini.

Leo nawakaribisha tujadili kwa pamoja juu ya hizi options mbili katika ya kumiliki mjengo kwa kununua au kwa kujenga mwenyewe Je upi ni uamuzi wa busara.Kwa ajili ya kwueka mjadala SAWA ninaposema kununua mjengo namaanisha pia option ya kununua custom house kwa kuchagua ramani etc.

Karibuni kwa mjadala.
 
Ninachokiona hapo uamuzi wenye busara kwa kitanzania ni kujenga mwenyewe.​
Upande wa nyumba za kununua mara nyingi muuzaji huwa anathaminisha gharama za ujenzi kuanzia mwanzo hadi Mwisho hivyo ataongezea kiasi flani Kama faida ili aweze kuuza kwa faida.​

Kama gharama ya ujenzi kajenga kwa 30M huenda akauza kwa 35M+.​
Vilevile kama mtu binafsi kajenga tofauti na mashirika yanayojihusisha na ujenzi na uuzaji wa nyumba unaweza nunua halafu ukashindwa kuishi (Nyumba zingine huzindikwa na mmiliki).​

Nyumba zinazojengwa na mashirika (apartments) hizi huwa zinafanana mno unakuwa kama unaishi kota bora ujenge nyumba yako ya upekee.​
Kwa kuhitimisha bora kujenga kuliko kununua.
 
Labda ununue uifanyie marekebisho makubwa.

Ila ni ngumu kupata nyumba yenye standards zako.

Na ni vyema ukafahamu hiyo nyumba imejengwaje, wengine wanaweka material below standards mwishowe uingie gharama kuvibadilisha.
 
Kama una mda wa kusimamia Ujenzi wa nyumba yako, basi jenga. Kama huna mda wa kusimamia Ujenzi wa nyumba yako, basi nunua.

ANGALIZO: Ukiona ni heri kununua kuliko kujenga, basi hakikisha unapata ABCs (info) za kutosha kuhusu nyumba hiyo unayotaka kununua. Sababu zingine zinakuwa na mauza uza, zingine siyo imara, zingine zinakuwa katika migogoro.
 
Hebu mcheck huyu mwenzako then utapata jibu.
IMG-20201005-WA0055.jpg
 
Kama una mda wa kusimamia Ujenzi wa nyumba yako, basi jenga. Kama huna mda wa kusimamia Ujenzi wa nyumba yako, basi nunua.

ANGALIZO: Ukiona ni heri kununua kuliko kujenga, basi hakikisha unapata ABCs (info) za kutosha kuhusu nyumba hiyo unayotaka kununua. Sababu zingine zinakuwa na mauza uza, zingine siyo imara, zingine zinakuwa katika migogoro.

Ni kweli mkuu. Kuna rafiki yangu alinunua nyumba ila gharama ya marekebisho ambayo ameshafanya mpaka sasa zinakaribiana na kujenga nyumba mpya na hajaweza kuhamia bado.
 
Ndugu zangu;

Kwa desturi yetu sisi watanzania,kumiliki mjengo ni moja kati aya ndoto za watu wengi na pia ni kama kipimo cha kiwango cha ukwasi(Networth).Katika kutafuta maisha wengi wetu tunafikiri kwamba kupanga nyumba ni umaskini.

Leo nawakaribisha tujadili kwa pamoja juu ya hizi options mbili katika ya kumiliki mjengo kwa kununua au kwa kujenga mwenyewe Je upi ni uamuzi wa busara.Kwa ajili ya kwueka mjadala SAWA ninaposema kununua mjengo namaanisha pia option ya kununua custom house kwa kuchagua ramani etc.

Karibuni kwa mjadala.
Kwa nyumba ya kuishi wewe na familia ambayo ndio unategemea utaishi hapo maisha yako yote, nadhani ni bora kujenga. Hii itakufanya uzingatie ubora na viwango unavyotaka kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

Pia unapojenga mwenyewe ni rahisi kuona mapungufu na kuyarekebisha mapema. Pia nafikiri ukijenga nyumba mwenyewe unaipenda zaidi na unajisikia uko nyumbani kuliko ukinunua.
 
Back
Top Bottom