Duu! Watu wanaongelea nyumba, wewe unaleta mambo ya gari.Galri unalo?
Kama una mda wa kusimamia Ujenzi wa nyumba yako, basi jenga. Kama huna mda wa kusimamia Ujenzi wa nyumba yako, basi nunua.
ANGALIZO: Ukiona ni heri kununua kuliko kujenga, basi hakikisha unapata ABCs (info) za kutosha kuhusu nyumba hiyo unayotaka kununua. Sababu zingine zinakuwa na mauza uza, zingine siyo imara, zingine zinakuwa katika migogoro.
Kwa nyumba ya kuishi wewe na familia ambayo ndio unategemea utaishi hapo maisha yako yote, nadhani ni bora kujenga. Hii itakufanya uzingatie ubora na viwango unavyotaka kuanzia mwanzo mpaka mwisho.Ndugu zangu;
Kwa desturi yetu sisi watanzania,kumiliki mjengo ni moja kati aya ndoto za watu wengi na pia ni kama kipimo cha kiwango cha ukwasi(Networth).Katika kutafuta maisha wengi wetu tunafikiri kwamba kupanga nyumba ni umaskini.
Leo nawakaribisha tujadili kwa pamoja juu ya hizi options mbili katika ya kumiliki mjengo kwa kununua au kwa kujenga mwenyewe Je upi ni uamuzi wa busara.Kwa ajili ya kwueka mjadala SAWA ninaposema kununua mjengo namaanisha pia option ya kununua custom house kwa kuchagua ramani etc.
Karibuni kwa mjadala.