Hili suala nilijaribu hata sabasaba wanieleze lakini ilikua ngumu kwangu kuielewa ,waka niambia habari hiyo hiyo katika kila shilingi mia sijui wanakupa kumi.
Nilisha wahi kweneda kwnye fixed deposit nikiwa na pesa yangu ya maana nikidhani wanapo sema at 2% interest basi nikajua una calculate hivi , 10,000,000 x0.02=200, nikajua unakula 200,000 kiulaini, kumbe ni kama kama hivi 10,000,000 x0.02/30 = 6,666.6666667 kumbe hako ka elf sita ndio unacho pata .
Tuache yote na misamiati na habari ndefu ambazo wengine ni ngumu kuzielewa.Twende practical kwa manufaa ya wengi. Mfano mimi nina shilingi 10,000,000 , nika nunua tBills je nina calculate vipi ? naomba jibu uwe umekdiria hiyo intest rate na pia uonyeshe ukokotoaji wote angalau tupate idea, Kila siku tuna ona stock exchange kwenye TV ila kuzielewa ni ngumu pia ,tunaomba msaada wenu asanteni.